Waislamu duniani wanaadhimisha Eid-ul-Fitr leo Ijumaa baada ya kuonekana kwa mwezi mpevu siku ya Alhamisi jioni, kuashiria kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. lakini baadhi ya nchi zitaadhimisha sikukuu hiyo kesho Jumamosi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Sherehe za Eid ul-Fitr mwaka huu zinafanyika siku ya Ijumaa, tarehe 20 au tarehe 21 Jumamosi kwa mataifa mengine.

Sherehe hizi ni mojawapo wa sherehe muhimu katika kalenda ya Kiislamu, na huadhimisha kutamatika kwa mwezi wa Ramadhan.

Eid El-Fitri ni miongoni mwa sikukuu kubwa na zenye heshima kubwa katika Uislamu, ikija mara moja kila mwaka baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ni siku ya furaha, shukrani na mshikamano kwa Waislamu duniani kote baada ya mwezi mzima wa ibada, kujinyima na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Katika siku hii muhimu, Waislamu husherehekea kwa nyoyo zilizojaa furaha, wakikumbuka mafanikio ya kufunga na kufanya ibada mbalimbali. Pia ni wakati wa kuimarisha mahusiano ya kifamilia na kijamii kupitia ziara, sadaka na kushirikiana chakula.

Kwa wengi, Eid ni zaidi ya sherehe; ni siku ya kuonesha ucha Mungu, upendo na mshikamano kwa jamii. Watu huvaa nguo nzuri, kuandaa vyakula maalum na kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki.

Katika mataifa ya Afrika, Eid ul-Fitr husherehekewa na swala, mlo, na utamaduni wa familia kujumuika pamoja.

Eid ul-Fitr husherehekewa mwisho wa mwezi wa Ramadhan ikiendana na mwezi wa tisa ya kalenda ya kiislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *