Israeli imeahidi kujizuia kutekeleza mashambulio dhidi ya miundombinu kuu ya gesi nchini Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Israel imejiri baada ya Iran kuanza kushambulia maeneo ya gesi na mafuta katika nchi za ghuba kujibu shambulio la Israel kwenye kituo chake cha gesi.

Qatar nayo imetupilia mbali madai ya Iran kwamba mashambulio ya Jumatano ya wiki hii kwenye miundombinu yake ya gesi yalilenga vituo vinavyohusishwa na marekani.

Iran ilishambulia kituo cha gesi cha Ras Laffan nchini Qatar kwa kile ilisema ni kujibu mashambulio ya Israeli kwenye kituo chake cha gesi cha Pars Jumatano (Machi 18).

Bei ya nishati ilipanda siku ya Alhamisi baada ya shambulio dhidi ya mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya gesi asilia duniani na kusababisha uharibifu ambao Qatar ilisema unaweza kuchukua miaka mitano kurekebishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *