Mbunge wa Jimbo la Segerea Agnesta Lambert Kaiza ameendelea kuonesha moyo wa kujali jamii kwa kutoa msaada wa vyakula, vifaa vya shule pamoja na fedha taslimu kwa watoto yatima, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kusherehekea Sikukuu ya Eid.
Msaada huo umetolewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha AL Hidaya kilichopo kata ya Mnyamani, jijini Dar es Salaam, ambapo mbunge huyo amesisitiza kuwa malezi na ustawi wa watoto yatima ni jukumu la jamii nzima, si la taasisi pekee.
Amesema utoaji wa vifaa vya shule unalenga kuinua viwango vya elimu kwa watoto hao, huku akihimiza wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia makundi yenye uhitaji.
(Feed generated with FetchRSS)