#HABARI: Mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini Jaji Mstaafu Julie Catherine Manning amefariki dunia leo katika Hospitali ya Hitech Sai Healthcare Upanga jijini Dar es Salaam alikokuwa akipata matibabu.

Jaji Mstaafu Manning aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 1973 hadi1975 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria kuanzia mwaka 1997 hadi 1983.

Julie Manning aliwahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu wa kwanza mwanamke Afrika Mashariki na kati pia aliwahi kuwa waziri wa Sheria.

Bi. Manning pia ni mmoja wa wanafunzi kumi na wanne wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *