#HABARI: Vikosi vya usalama vya Israel vimeripotiwa kuwashambulia kwa mabomu ya machozi waumini wa Kiislamu waliokuwa wakijaribu kutekeleza Swala ya Eid karibu na eneo la Msikiti wa Al-Aqsa jijini Jerusalem.

Hatua hiyo imelenga kuzuia mikusanyiko ya waumini hao katika eneo hilo takatifu ambalo limefungwa na mamlaka za Israel tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Tukio hilo limetokea wakati waumini wakijaribu kutekeleza ibada hiyo muhimu ya Eid katika maeneo ya wazi yanayozunguka msikiti huo, kufuatia amri ya kuzuia kuingia ndani ya Al-Aqsa.

Mashuhuda wameeleza kuwa hali ilikuwa ya taharuki huku moshi wa mabomu ya machozi ukitanda maeneo hayo, jambo ambalo limezua ukosoaji mkubwa wa kimataifa kuhusu haki ya kuabudu wakati wa migogoro ya kijeshi inayozidi kushika kasi katika ukanda huo.

Kufungwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa kunatajwa kuwa sehemu ya hatua kali za kiusalama zilizochukuliwa na Israel tangu kuanza kwa operesheni za kijeshi dhidi ya miundombinu ya Iran.

Hata hivyo, viongozi wa kidini na mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa kuzuia ibada katika siku kuu kama ya Eid kunaweza kuchochea hasira zaidi miongoni mwa Wapalestina na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *