Moshi, Kilimanjaro Machi 22, 2026, Wanariadha wa Kitanzania wameendelea kung’ara katika ardhi ya nyumbani, kupitia mbio za kilomita 21 maarufu ‘Yas Kili International Half Marathon 2026’.
Mbizo hizi zinazofanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro ni moja ya matukio makubwa ya michezo barani Afrika.
Akizungumza wakati wa kuwapongeza washiriki, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, alisema mbio za mwaka huu zimeonyesha namna Watanzania wanavyoinuka na kuthibitisha uwezo wao katika riadha.
Waziri Makonda alisema: “Kile kilichofanyika Moshi leo sio tu mashindano; ni uthibitisho wa kujituma, uzalendo na uwezo mkubwa wa Watanzania kushindana na kuibuka na ushindi.
Waziri Makonda pia aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amehahidi kuwa mgeni rasmi kwa mashindo ya Kili Marathon kwa mwaka ujao huku pia akiahidi kuongeza dau nono la shilingi milioni 100 za kitanzania kwa washindi.
Yas Kili International Half Marathon imeendelea kuwa jukwaa muhimu linalounganisha watu, kukuza utalii na kuleta hamasa mpya katika sekta ya michezo nchini.”
Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton Bacara, alisema ushindani ulioonekana katika mbio za kilomita 21.1 umedhihirisha ubora wa wanariadha wa Tanzania na nguvu ya hamasa inayozidi kukua kila msimu.
Bacara alisema udhamini wa zaidi ya miaka 12 wa kipengele cha Yas Half International Marathon unatokana na dhamira ya Yas kuwa mshirika wa maendeleo ya michezo nchini. Kaulimbiu ya mwaka huu ya “Kila Kona, Kila Hatua Kasi Zaidi,” inaakisi juhudi za kampuni kuhakikisha huduma za mawasiliano ya 4G na 5G zinawafikia Watanzania kote nchini.
Alisema, “Kwa mwaka wa tatu mfululizo tumetambuliwa na kampuni ya kimataifa ya Ookla kama mtandao wenye kasi zaidi nchini Tanzania. Tunaendelea kuwekeza katika miundombinu ili kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na mawasiliano ya uhakika -iwe ni biashara, elimu, kilimo au kusherehekea mafanikio ya ushindi wa mbio kama hizi za Yas Kili International Half Marathon mtandaoni.”
Katika upande wa mazingira, Bacara alisisitiza dhamira ya Yas kuendeleza mradi wa Yas Green for Kili, unaolenga kulinda na kurejesha uoto .
(Feed generated with FetchRSS)