Jaji mstaafu Julie Manning anatarajiwa kuzikwa Machi 24, 2026 katika Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, baada ya ibada ya kuaga mwili itakayofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Peter, Oysterbay.

Jaji Jilie alifariki dunia Machi 20 mwaka huu na anakumbukwa kama Jaji wa kwanza mwanamke nchini Tanzania, aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya sheria.

Ndugu, jamaa na marafiki wamemuelezea marehemu Manning kuwa kiongozi mwenye weledi, uadilifu na aliyejitolea kuhudumia jamii kwa moyo wote.

✍ Upendo Michael
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *