Tanzania Leo inaadhimisha ni siku ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) inayoadhimishwa kila 23 March ambapo Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuendeleza na kuhifadhi urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika kilichopo jijini Dar es Salaam pamoja na kulinda maeneo yote ya kihistoria yaliyotumika wakati wa mapambano ya ukombozi wa Afrika

‎Mipango hiyo imesemwa na Mwenyekiti wa Pan-African Women Organization ( PAWO ), Dkt. Susan Kolimba, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika yaliyofanyika katika kituo Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika ambapo amesema pamoja na mafanikio ya ukombozi wa kisiasa, bado kuna haja ya kuhakikisha kuwa uhuru huo unakuwa chachu ya mapinduzi ya kiuchumi barani Afrika,

‎Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Christopher Mhongole, amesema Tanzania imeendelea kuwa kitovu muhimu cha historia ya ukombozi wa Bara la Afrika

‎Na kuongeza kuwa kituo hicho kimeandaa mdahalo maalum unaowakutanisha wadau mbalimbali kujadili kwa kina historia na urithi wa ukombozi wa Afrika, kwa lengo la kuongeza uelewa kwa jamii.
‎Mhongole amesisitiza kuwa elimu hiyo itasaidia wananchi kutambua na kujivunia urithi wao, kushiriki katika kuuhifadhi, na kutumia historia hiyo kama chachu ya kujenga uzalendo na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *