Mahakama ya rufaa nchini Ufaransa, imesisitiza kuwa mwanasiasa wa upinzani Marine Le Pen alitumia fedha za Umoja wa Ulaya kwa matumizi yake binafsi, na ataendelea kutumikia kifungo jela licha ya kumpunguzia adhabu inayomkabili.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unaacha mwanya kidogo kwa mwanasiasa huyo wa siasa za mrengo wa kulia, kuwania urais mwaka 2027.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imemzuia Le Pen kutochaguliwa au kushika wadhifa wowote wa umma, kwa kipindi cha miezi 15 ambacho ameshakitumikia, huku akihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Katika adhabu hiyo, mwanasiasa huyo atakitumikia kifungo cha mwaka mmoja akiwa nyumbani, chini ya uangalizi maalum.

Hii inamaanisha kuwa, anaweza kuwania urais wakati Ufaransa itaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Aprili mwaka ujao, lakini atakuwa chini ya kifungo ambacho kitakuwa kikwazo kwake.

Le Pen, alikwenda kwenye Mahakama ya rufaa jijini Paris, baada ya mwaka uliopita kuhukumiwa jela miaka minne na kuzuiwa kuingia kwenye Ofisi ya umma kwa miaka mitano, baada ya kupatikana na hatia ya kufuja fedha za bunge la Umoja wa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *