Zaidi ya kaya 500 katika eneo la Sanya Stesheni lililopo Kata ya Kia, Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro zimeingirwa na maji kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha, hali iliyowalazimu baadji yao kushindwa kutoka nje ya makazi hayo kwenda kwenye shughuli za kujioatia kipato huku wanafunzi wakishindwa kwenda shule kutokana na kadhia hiyo.
Wananchi hao wamesema mafuriko hayo licha ya kuzingira makazi yao lakini pia yamesababisha uharibifu wa mashamba na mali nyinginezo hatua iliyowalazimu kuomba mamlaka kuweka Kizuizi Cha maji ikiwemo uwekwaji wa mkondo wa kutiririsha maji ili kuepusha athari inayoweza kuwabughudhi wananchi wanaolazimika kujifungia ndani kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
(Feed generated with FetchRSS)