Wakati vita vinaendelea kuyumbisha Mashariki ya Kati na kuongeza mateso kwa raia katika Ukanda huo, athari za kiuchumi za hali ya dharura bado zinaendelea kujitokeza, huku Mlango wa Bahari wa Hormuz ukiwa kitovu cha uangalizi wa kimataifa, bei ya mafuta ghafi ikipanda tena hadi zaidi ya dola 100 kwa pipa. Wakati huohuo, mashambulizi ya walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel yameongezeka kwa kiasi kikubwaumesema leo Umoja wa Mataifa.

Familia za Syria na Lebanon, ikiwa ni pamoja na watoto, wanawasili katika bandari ya Joussieh katika kijiji cha Rural Homs, Syria, Machi 10, 2026, baada ya kuvuka kutoka Lebanon. Kikundi hicho kinabeba mali, na mabasi na magari karibu. Wajumbe wa UNICEF wakiongozwa na Naibu Mwakilishi wa Programu Zeinab Adam wanatathmini hali na huduma zinazosaidiwa na UNICEF kwa familia zilizohamishwa.

© UNICEF/Ramadhan Sulayman

Watu wanavuka mpaka kutoka Lebanon kwenda Syria katika eneo la vijijini la Homs.

Watu 130,000 wakimbilia Syria

Zaidi ya watu 130,000 wamevuka kuingia nchini Syria na zaidi ya watu milioni moja wamekuwa wakimbizi wa ndani nchini Lebanon tangu mapema Machi, kutokana na mzozo wa Mashariki ya Kati, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.

Kwa mujibu wa shirika hilo harakati hizi kubwa za watu kufurushwa zinaongeza shinikizo kwa “jamii ambazo tayari ziko katika mazingira magumu na kuongeza mahitaji ya kibinadamu”.

Mkurugenzi Mkuu wa IOM, Amy Pope amesema “Mazingira ya sasa ni ukumbusho dhahiri wa jinsi ukosefu wa utulivu unavyoweza kubadilisha kwa haraka mifumo ya uhamaji katika kanda nzima.” 

Ameongeza kuwa “Watu wengi wanaohama tayari wanaishi katika hali dhaifu, na kadri shinikizo linavyoongezeka, mahitaji ya kibinadamu yataongezeka. Msaada endelevu wa kimataifa ni muhimu ili kuhakikisha watu hawa wanapata ulinzi na msaada wanaohitaji, popote walipo.”

Shirika hilo limesema watu wengi wanaowasili Syria ni familia na vijana wa kiume waliokuwa wamesafiri kwenda Lebanon kwa ajili ya kazi.

Maono ya panoramic ya jirani ya Silwan katika Yerusalemu Mashariki, kuonyesha majengo yenye msongamano mkubwa juu ya kilima chini ya anga la bluu wazi. Baadhi ya miundo inaonekana kuharibiwa au chini ya ujenzi, kuonyesha kuendelea kuhama na upanuzi wa makazi.

Familia za Wapalestina zinafukuzwa katika kitongoji cha Silwan katika Yerusalemu Mashariki.

Mkutano kuhusu maeneo yanayokaliwa ya Palestina 

Kikao cha asubuhi leo katika Baraza la Haki za Binadamu HRC, kimekamilika na kila mtu anaondoka katika Ukumbi mkubwa wa mikutano mjini Geneva Uswisi.

Katika Mkutano huo Bahrain kwa niaba ya nchi za Ghuba, imeomba mjadala wa dharura kuhusu vita vya Mashariki ya Kati kesho Jumatano saa 3 asubuhi zsaa za Geneva, baada ya kulaani mashambulizi yanayoendelea ya Iran.

Hii imekuja pamoja na mjadala uliopangwa kuhusu “Hali ya haki za binadamu katika eneo la Palestina na maeneo mengine ya nchi za Kiarabu yanayokaliwa kwa mabavu” unaojulikana pia kama Kipengele cha 7 ambao wakosoaji wa Baraza wanaupinga vikali wakisema unalenga kwa njia isiyo ya haki na kwa utaratibu nchi moja tu, katika hali hii Israel.

Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Nada Al-Nashif amezungumza pia katika mkutano huo mapema leo.

 Ameliezeza Baraza kuhusu kuendelea kwa upanuzi wa makazi ya Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu kabla ya kuwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na Israel.

media:entermedia_image:8a151129-5a0f-4d63-aeed-e99d1c4f6aa8

UNHCR Video

Mkimbizi wa Syria nchini Lebanon

Dawa za kuokoa zawasili Lebanon: WHO

Vifaa muhimu vya matibabu vimefika Lebanon, vikiwemo tani 3.5 za vifaa vya matibabu ya majeraha na dharura limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO.

Msaada huu unahitajika kwa dharura huku kukiwa na mashambulizi ya mabomu ya Israel dhidi ya malengo ya Hezbollah na amri za uhamishaji wa watu kwa wingi zinazoathiri jamii nzima kusini mwa Mto Litani na kusini mwa mji mkuu Beirut.

WHO inasema kuwa vifaa hivyo vitaendeleza huduma za kuokoa maisha katika hospitali, vituo vya afya ya msingi na vitengo vya afya tembezi.

WHO imepongeza jukwaa la misaada ya kibinadamu la Tume ya Ulaya (ECHO) kwa msaada huo.

Meli kubwa ya mizigo kusafiri kwenye Mto Mississippi karibu New Orleans, na anga bluu mawingu juu.

UN News/Daniel Dickinson

Kufungwa kwa mlangobahari wa Hormuz kunaathiri biashara kwa kiwango cha kimataifa.

Njia ya kibinadamu yahitajika Hormuz

Takriban mabaharia 20,000 wameathiriwa na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati na msongamano wa usafirishaji uliotokea kutokana na vita hivyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO), kumekuwa na mashambulizi 18 dhidi ya meli zilizokuwa zikijaribu kupita katika Mlango wa Bahari wa Hormuz ambayo ni njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta na gesi kwenda sehemu mbalimbali duniani kati ya tarehe 1 Machi na 19 Machi.

Katika kikao cha dharura kilichofanyika wiki iliyopita mjini London kukabiliana na mgogoro huo, Katibu Mkuu wa IMO, Arsenio Dominguez, alizihimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zenye meli mashariki mwa Mlango wa Hormuz “kutochukua hatari zisizo za lazima katika kusafiri kuelekea magharibi. Hatupaswi kuwaweka mabaharia katika hatari kubwa zaidi ya wanayokumbana nayo sasa.”

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limehimiza kuanzishwa kwa njia ya kibinadamu “ya kuhamisha meli zote na mabaharia ambao kwa sasa wamekwama.” Inaeleweka kuwa mazungumzo yanaendelea na nchi wanachama na wadau wengine walioathiriwa na mgogoro huo.

Kamishina Mkuu wa UN wa Haki za Binadamu akihutubia Baraza la Haki za Binadamu Gebeva Uswisi

Kamishina Mkuu wa UN wa Haki za Binadamu akihutubia Baraza la Haki za Binadamu Geneva Uswisi

Baraza la Haki za Binadamu

Mjadala wa dharura  kuhusu Iran utakaofanyika kesho Jumatano katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ni tukio la nadra na ni mara ya 11 tu tangu jukwaa hilo kuanzishwa mwaka 2006, jambo linaloonesha athari kubwa ya kimataifa ya vita vya Mashariki ya Kati.

Katika mjadala huo utakaodumu kwa saa tatu, tunatarajia kusikia kutoka kwa maafisa wakuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR), pamoja na wataalamu huru walioteuliwa na Baraza, wanadiplomasia wakuu wanaowakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa Geneva, pamoja na asasi za kiraia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *