Seneta wa chama cha Democratic cha Marekani, Chris Murphy, amesema katika ujumbe wake: “Vita na Iran ni vita vya kijinga zaidi katika historia ya Marekani.”

Katika ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii, Chris Murphy, seneta wa chama cha Democratic cha Marekani, ameashiria mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na kuandika: “Hatujawahi kuona kiwango hiki cha kukosa ustahili na kujimudu katika vita katika historia ya Marekani.”

Seneta huyo wa Marekani pia amesema katika ujumbe mwingine: “Tunatumia dola bilioni 2 kwa siku kwa ajili ya kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, mlango-bahari uliokuwa wazi kabla ya vita; huu ni wendawazimu.”

Wakati huo huo, Seneta wa Kidemokrati wa Marekani, Andy Kim, amepinga sera za kuchochea vita za rais wa nchi hiyo, Donald Trump akiashiria mauaji ya askari wa Marekani katika vita dhidi ya Iran na kusisitiza kwamba ni lazima tupunguze gharama mara moja.

Andy Kim ameongeza katika ujumbe wake kwenye mitandao wa kijamii wa X kwamba: “Bei ya petroli imeongezeka nchini Marekani, wanajeshi wa Marekani wameuawa, na hakuna uwezekano wa vita hivi kuisha hivi karibuni.”

Sambamba na hayo vyombo vya habari vya Marekani vinaendelea kufichua kwamba mamia ya wanajeshi wa nchi hiyo wanaendelea kuuawa na kujeruhiwa katika vita vilivyoanzishwa na nchi hiyo ikishirikina na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *