
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa onyo kali kuhusu mpango wa pamoja unaolenga kutwaa kisiwa cha Iran, mpango unaoungwa mkono na mshirika wa kikanda wa maadui.
Katika chapisho aliloweka kwenye ukurasa wake wa X siku ya Jumatano, Qalibaf alitoa onyo zito kuhusu uwezekano wa operesheni ya kukalia kwa mabavu moja ya visiwa vya kimkakati vya Iran, akisema kuwa maadui wa nje wanashirikiana na nchi jirani ili kutekeleza ajenda yao ya uhasama.
Qalibaf ameonya kuwa: “Ikiwa watathubutu kuchukua hatua hata moja, miundombinu yote nyeti ya nchi hiyo ya kikanda itakuwa shabaha ya mashambulizi bila mipaka.”.
Tawala za kigaidi za Marekani na Israel zilianzisha vita vya kichokozi dhidi ya Iran kwa kumuua shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khamenei, pamoja na makamanda kadhaa waandamizi wa kijeshi na raia mnamo Februari 28 sawa na 10 Ramadhani. Tokea wakati huo, tawala hizo za kijinai zimeua idadi kubwa ya raia wasio na hatua, wakiwemo watoto wa shule, kushambulia mahospitali na miundombinu ya raia na pia vituo vya kijeshi na usalama.
Katika kujibu jinai hizo, Vikosi vya Ulinzi vya Iran vinaendeleza operesheni za kulipiza kisasi, vikilenga ngome za kijeshi na kiuchumi za Israel na za Marekani katika ardhi za baadhi ya nchi za eneo.