
Msemaji mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa, kulingana na makadirio ya kijeshi ya Iran, mamia ya wanajeshi wa Marekani pamoja na zaidi ya Waisraeli 1,300 wameuawa katika vita vinavyoendelea ambavyo, vilianzishwa na tawala hizo mbili dhidi ya Iran.
Katika mahojiano mapana yaliyotangazwa na Chaneli ya Habari wa Televisheni ya Taifa ya Iran, Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi alithibitisha taarifa za hasara kubwa miongoni mwa wanajeshi wa Marekani, akisema makadirio yanaonyesha kati ya wanajeshi 600 hadi 800 wa Marekani wameuawa, huku karibu wengine 5,000 wakijeruhiwa.
Aidha, jenerali huyo alinukuu vyanzo vilivyoko ndani ya Israel vikisema kuwa wanajeshi 1,321 wa Israel wameuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Iran. Amebainisha kuwa huenda idadi hiyo ni ndogo kuliko hali halisi, kwani utawala wa Israel umekuwa ukipunguza ukubwa wa hasara zake katika vita hivyo.
Pia amesema Iran inaendelea kufuatilia kwa karibu harakati za majeshi ya Marekani katika eneo lote la Asia ya Magharibi, akisisitiza kuwa muundo wa kijeshi wa Marekani katika eneo hilo “umeporomoka kwa muda mfupi sana.”
Brigedia Jenerali Shekarchi amekosoa vikali chokochko na uchokozi wa jeshi la Marekani katika eneo la Asia Magharibi, huku akifafanua kuhusu hatua za Iran kujibu mashambulizi yanayoendelea dhidi yake.
Amefichua kuwa wanajeshi wengi wa Marekani sasa wamelazimika kuondoka katika baadhi ya kambi zao za kijeshi na kutafuta hifadhi katika hoteli za kiraia katika nchi za eneo, hatua aliyokosoa akisema ni jaribio la kutumia majengo ya kiraia kama ngao ya shughuli za kijeshi.
Brigedia Jenerali Shekarchi ameongeza kuwa: “Tumebomoa kambi 17 za Marekani katika eneo hili, na wameshindwa kulinda wanajeshi wao na miundombinu yao na hilo ni pigo kubwa kwa haiba na itibari ya Marekani.”
Msemaji huyo pia amesisitiza kuwa doktrini ya kijeshi ya Iran inalenga hasa kujibu uchokozi, na kwamba Iran haitaki kuanzisha migogoro isiyo ya lazima.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa azma ya Iran haitayumba kukabiliana na uingiliaji wa kigeni unaoendelea.
Akiashiria masharti yaliyotolewa na Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, amesema vikosi vya Iran viko tayari kuyalinda.
Amesema hali ya Lango-Bahari la Hormuz haitarudi tena kuwa kama ilivyokuwa hapo awali,
Jenerali huyo amesisitiza tena kuwa hatua za kijeshi za Iran zinalenga kulinda mamlaka na uhuru wa nchi pamoja na kuhakikisha usalama wa eneo na kushambulia raia wasio na hatia.
Msemaji mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesisistiza kuhusu azma ya Iran ya kuendelea na mapambano hadi malengo yake yatakapofikiwa.