Ndoto za vijana zimeanza kudhihirika kwa vitendo baada ya kikundi cha “Vijana Ujenzi Workshop Yard” kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kunufaika na mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya shilingi milioni 80 inayotolewa na serikali chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan.

Kupitia mkopo huo, vijana hao wamefanikiwa kukuza shughuli zao za uzalishaji na kuimarisha hali zao za kiuchumi. Mafanikio hayo yamewawezesha si tu kujikwamua binafsi, bali pia kurejesha kwa jamii kwa kutoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa shule za eneo hilo, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Benton Albert, amesema mkopo huo umeleta mabadiliko makubwa kwa wanachama, wengi wao wakifanikiwa kujitegemea kiuchumi, kumiliki mali na kuendeleza biashara zao.
“Sisi kikundi chetu cha Vijana Ujenzi workshop Yard tulinufaika tukapata mkopo wa milioni 80, ambapo kwenye mkopo huo mpaka sasa tumesharejesha milioni 73.4 na tumenufaika kwa mkopo huo ambapo vijana wengi wameweza kujikwamua kiuchumi, wameweza kuendesha maisha yao na kupata vitu mbalimbali. Baadhi ya vijana hapa wamefanikiwa kupata viwanja, nyumba na biashara ikawa imesimama vizuri” Benton Albert, Mwenyekiti Vijana Ujenzi Workshop Yard

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *