Tozo 628 zapunguzwa kuinua biasharaTozo 628 zapunguzwa kuinua biashara

RAIS wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema mazingira ya biashara nchini Tanzania yameendelea kuimarika kwa kiwango kikubwa kufuatia hatua za serikali kuondoa vikwazo vya kisheria na kikodi vilivyokuwa vikiwakwamisha wafanyabiashara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uhakiki wa rasimu ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II), Dk. Mwinyi ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na uongozi na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na ushirikiano wa karibu kati ya serikali na wadau wa maendeleo.

Amesema katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya MKUMBI, serikali imefanikiwa kufuta au kupunguza zaidi ya ada, tozo na kodi 628 zilizokuwa zikikwamisha ukuaji wa sekta mbalimbali, ikiwemo viwanda, madini, kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.

Aidha Rais Mwinyi amebainisha kuwa mapitio ya zaidi ya sheria 94 yamefanyika kwa lengo la kuondoa mwingiliano wa majukumu miongoni mwa taasisi za serikali, hatua iliyosaidia kupunguza urasimu na kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara. SOMA: Rais Mwinyi azitaka taasisi za biashara kuondoa urasimu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *