Mwanaume Mmoja aliyefahamika kwa jina la Bunzali Jidola (30) Mkazi wa kata ya mwamakona Wilaya ya Igunga mkoani anadaiwa kumuua mtoto wake mchanga wa kike mwenye umri wa miezi miwili kwa kumchinja na kitu chenye nchi kali na kisha kumjeruhi mke wake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili wake na kukimbilia kusikojulikana na baada ya msako kufanyika akakutwa amejinyonga katika nguzo ya umeme Wilayani hapo.
Inaelezwa kuwa chanzo cha awali cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifanya mauaji hayo baada ya kuhisi kuwa mtoto huyo sio wake hali iliyosababisha kufanya tukio hilo na hapa Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao aneleza hali halisi.
Hata hivyo mke wa marehemu huyo ambaye alijeruhiwa alifikishwa katika hospitali ya nkinga Wilaya hapo akiendelea na matibabu huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora akitoa wito kwa wananchi kutafuta suluhisho la migogoro ya kifamilia kwa njia za amani.
Katika hatua nyingine wakazi wa mkoa wa Tabora wameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa afya ya akili sawa na kulitaka Jeshi la Polisi mkoani hapa kuendelea kuwadhibiti wahalifu wa matukio mbalimbali ili mkoa uwe katika hali ya usalama na amani.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)