Muuguzi akiwa na bendera ya Ghana anafuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru katika jumba la Jubilee House tarehe 6 Machi 2025 mjini Accra.

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya kuvunja shirika kuu la Marekani la kutoa msaada wa kigeni mwaka jana, utawala wa Trump umeanza tena kutoa mamilioni ya dola kwa nchi za Afrika ili kusaidia miundo yao ya huduma za afya na kusaidia kupambana na magonjwa.

Lakini misaada hiyo inakuja na mikataba mipya ambayo inapingwa na baadhi ya mataifa kutokana na masharti yaliyofungamana nayo.

Wakati makubaliano ya awali yalipotiwa saini na Rais wa Kenya William Ruto huko Washington mwezi Desemba mwaka jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema anatuimai yatakuwa ya kwanza kati ya mingine mengi.

“Tunatarajia kusaini, sijui, 30, 40, na ngapi? au Hamsini? Naam, hii ni ya kwanza. Tutakumbuka hili kila wakati … na tunafikiri tumemchagua mshirika kamili,” Rubio alitangaza.

Lakini hata makubaliano hayo muhimu ya thamani ya dola bilioni 2.5 (£1.9bn) yaliyofikiwa na Kenya, yamecheleweshwa na wanaharakati waliokwenda mahakamani kuizuia, japo mawaziri hatimaye waliidhinisha mwezi uliopita.

Muda mfupi baada ya kuchukua hatamu ya uongozi, Rais Donald Trump aliamuru kufungwa kwa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) huku kukiwa na shutuma za upotevu, katika mchakato wa kuangamiza programu za afya katika baadhi ya nchi za Afrika ambazo zilitegemea ufadhili wa Marekani.

Mkakati mpya wa afya wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje unahitaji serikali zinazopokea misaada kushiriki uwajibikaji kwa kuongeza matumizi yao ya afya, kwa lengo la kujenga mifumo imara ambayo hatimaye inaweza kujitegemea. Kwa mfano, ni kuchangia dola bilioni 1.6 kwa makubaliano ya jumla na Kenya – huku taifa hilo la Afrika Mashariki likiahidi dola milioni 850 kwa kipindi cha miaka mitano.

Utawala wa Trump unatumai kwamba kushirikiana na uongozi wa kitaifa kutaboresha uhusiano wa jadi wa wafadhili na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo inasema yaliunda utegemezi, uliosababisha mipango sambamba ya utoaji na kunyonya wa fedha za misaada kwa gharama za ziada.

Marco Rubio (kulia) na Rais wa Kenya William Ruto (kushoto), wakiwa wamevalia suti nyeusi na tai, wakipeana mikono jijini New York mnamo Septemba 2025 mbele ya bendera za Kenya na Marekani.
.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

“Msaada wetu kwa nchi hizo hautakuwa tu dola zinazosambazwa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo kisha itaingia nchini na kulazimisha programu,” Rubio aliambia kamati ya bunge mwezi uliopita.

“Sio tu kwamba tunatibu hali kali za watu wagonjwa, bali tunawasaidia kujenga uwezo na uwezo wa kufanya hivi wenyewe.”

Lakini matokeo yake ni mabadiliko kutoka kwa mfumo wa ushirikiano wa kimataifa uliowekwa katika Shirika la Afya Duniani (WHO), ili kuelekeza makubaliano na serikali za kibinafsi ambazo zinahusiana na maslahi ya kimkakati na kibiashara ya Marekani.

Marekani ilijiondoa WHO mapema mwaka huu ikisema haikuwa haki kwamba Washington ilitoa ufadhili mwingi zaidi kuliko nchi zingine na kudai kwamba shirika hilo lilisimamia vibaya janga la Covid-19, halina uwazi, na lilikuwa katika hatari ya kuingiliwa kisiasa.

Kwa hali ambayo inaibua utata, mikataba ya pande mbili ya Marekani inakuja na masharti ya kuyapatia kipaumbele makampuni ya dawa na mashirika ya matibabu ya Marekani kutengeneza na kutoa matibabu.

“Mpango wetu wa kimataifa wa usaidizi wa afya wa kigeni si msaada tu – ni utaratibu wa kimkakati wa kuendeleza maslahi yetu ya pande mbili kote duniani,” inasema hati ya sera.

Nchi 32 zilikuwa zimekubali Makubaliano ya Mpango huo waa Afya (MOU) kufikia katikati ya Mei, Amerika Kusini, Caribean na takribani nchi 20 barani Afrika. Lakini baadhi – kama vile Ghana, Zimbabwe na Zambia – zimekataa kujisajili, zikitoa sababu tofauti.

Nchini Zambia, Waziri wa Mambo ya Nje Mulambo Haimbe alikosoa kile alichokielezea kama juhudi za Marekani za kuunganisha ufadhili wa afya na maslahi ya kiuchumi ya Marekani kwa kuunganisha makubaliano hayo na makubaliano tofauti yanayoipa Washington ufikiaji wa madini muhimu.

“Wenzetu [Marekani] walikuwa na mtazamo kwamba [mikataba hiyo miwili] lazima ichukuliwe kama kifurushi cha kujadiliwa na kuhitimishwa kwa wakati mmoja maalum,” aliiambia BBC, akisema serikali ya Zambia ilitaka kuijadili tofauti kwa maslahi yake.

“Marekani ilihisi kwamba kuna haja ya kuwa na upendeleo katika matumizi ya madini muhimu. Na mfumo ulikuwa ni kuakisi hilo,” aliongeza.

Wizara ya Mambo ilielekea kuunganisha masuala hayo mawili ilipohojiwa na BBC lakini ilitoa jibu thabiti la “Marekani Kwanza”.

“Utawala wa Trump umeweka wazi, usaidizi wa kigeni wa Marekani si hisani – bali ni mtaji wa kimkakati unaopaswa kuwekezwa kwa busara ili kuendeleza maslahi ya Marekani – na tunatarajia washirika wetu wote na mataifa yanayopokea kuchukulia kwa uzito vipaumbele vya kimkakati na kibiashara vya Marekani,” msemaji wa idara alisema.

Afisa wa utawala aliunganisha hatua hiyo na “kushindwa kwa Pretoria kufanya maendeleo yanayoonekana kuhusu maombi ya sera”, ikiwa ni pamoja na jinsi inavyoonekana jinsi jamii ya Waafrikana weupe walio wachache inavyoshughulikia suala hilo. Marekani inadai kwamba “mauaji ya kimbari ya wazungu” yanafanyika Afrika Kusini na yamepuuzwa sana.

Kwa baadhi ya nchi za Afrika ambazo zilikuwa zikifanya mazungumzo ya makubaliano ya pande mbili, ilikuwa ni wasiwasi kuhusu upatikanaji wa data za afya wa Marekani ambao ulisababisha kengele za tahadhari. Hii ilijumuisha taarifa za wagonjwa pamoja na rasilimali za kibiolojia zinazojulikana kama vimelea – viumbe vinavyosababisha magonjwa kama vile virusi, bakteria na vimelea.

Mkono wa mtu aliye na maambukizi ya VVU nchini Zimbabwe ukiwa umeshikilia pakiti ya vidonge alivyopokea kama sehemu ya matibabu yake jijini Harare - Juni 2019.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Mahakama ya Kenya awali ilisitisha makubaliano ya nchi hiyo baada ya pingamizi la kisheria kutilia shaka ulinzi wa faragha ya mgonjwa.

Arnold Kavaarpuo, mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Ulinzi wa Data ya Ghana, aliiambia BBC kwamba serikali huko Accra ilipinga makubaliano hayo kwa sababu kama hizo.

“Tulikuwa na wasiwasi kuhusu wigo na upana wa data uliokuwa ukihitajika,” alisema.

“Ilikuwa sisi tukusanye data na kuipeleka kwa mamlaka ya Marekani, bila ya kuhakikishiwa ulinzi wa data ya Ghana na uhuru wa Ghana.

“Na kutokana na hilo kwa mtazamo wetu,” aliongeza, “tulihisi data inapoondoka kwenye mipaka ya Ghana, hatukuwa na udhibiti wa kitakachotokea.”

Zimbabwe pia ilitaja wasiwasi kuhusu maombi ya data ya matibabu, ambayo huenda ingetolewa kwa makampuni ya dawa ya Marekani, kama sababu iliyoifanya kukataa mpango huo wa Marekani.

Hakukuwa na dhamana kwamba dawa au chanjo zilizotengenezwa kutokana na vimelea zingepatikana kwa watu wake, msemaji wa serikali alisema, akibainisha kuwa WHO tayari ilikuwa na mfumo wa wanachama kushiriki data na kufaidika na matibabu yoyote katika magonjwa yajayo ya milipuko .

Nchi za Afrika zimekuwa zikiwasilisha taarifa za matibabu kupitia mipango iliyopo ikiwa ni pamoja na USAID na Pepfar, mpango mkuu wa Marekani wa kukabiliana na VVU na Ukimwi.

Marekani inasisitiza kwamba kuwasilisha data na sampuli ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya kisayansi na ushirikiano wa pamoja.

Na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema nyenzo zilizoombwa ni data ile ile iliyokusanywa na isiyotambuliwa ambayo imetumika kwa miaka mingi katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza.

Kilichobadilika ni muktadha, anasema Nelson Aghogho Evaborhene, msomi wa PhD katika utawala wa afya duniani katika Chuo Kikuu cha Roskilde nchini Denmark.

“Ilikuwa uhusiano usio sahihi, lakini ulikuwa wa kustahamiliana kisiasa,” anasema, “kwa sababu ungeweza kuunadi kwa watu wa ndani kama hitaji la kujitolea la kuboresha huduma ya afya.

“Lakini sasa imebadilika sana, kwa sababu ni hatua ya kujinufaisha kutokana na miamala.”

Mataifa mengi ya Afrika pia yamepata funzo kutoka kwa Covid, kwani mbio za kutafuta chanjo zilithibitisha thamani ya data ya vimelea lakini ziliacha bara hilo likipambana kuwatatutia chanjo watu wake.

“Nadhani moja ya fursa zetu kubwa kama Afrika,” anasema Aggrey Aluso, mkurugenzi mtendaji wa Resilience Action Network Africa (Rana), “ni kwamba tuna taarifa muhimu ambazo zinaweza kusaidia kujenga mfumo ikolojia wa usalama wa afya duniani.”

Rana alijiunga na zaidi ya vikundi 50 vya asasi za kiraia kutia saini barua ya wazi akiwaonya viongozi wa Afrika kwamba masharti ya Marekani hayaendani na maslahi ya kitaifa au kikanda ya Afrika, mtazamo unaoungwa na Afrika Kusini.

“Kusema ukweli, hakuna taifa duniani linalojiheshimu linaloweza kukubaliana na masharti hayo [mawili],” Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Dkt. Aaron Motsoaledi aliiambia BBC.

“Kwamba [Marekani] itapata vimelea vyao ikiwa kuna janga lolote au janga katika eneo lao.

“Na pia watawapa jenomu ya maisha. Lakini Marekani itawapa pesa kwa miaka mitano.”

Mjadala kuhusu diplomasia ya afya umepunguzwa kasi katika wiki za hivi karibuni kufuatia kuenea kwa mlipuko mpya wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Amadou Bocoum

Amadou Bocoum

When this new Ebola came, the staffing was not there, and the emergency stock that we also used to have was also not there”

Amadou Bocoum
Care’s country director in DR Congo

DR Congo ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza kukubali mikataba mipya ya afya ya Marekani – na Marekani inasema makubaliano hayo yanasaidia kuratibu mwitikio wa Kinshasa kwa mgogoro huo.

Lakini, kulingana na wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kiutu na maafisa wa zamani wa afya wa Marekani, kupunguzwa kwa misaada ya Marekani kwa DR Congo na WHO kulidhoofisha sana mwitikio wa kukabiliana na magonjwa.

Amadou Bocoum, mkurugenzi wa nchi wa DR Congo wa shirika la Care International, anasema ilibidi awafute kazi wafanyakazi 36 – theluthi moja ya wafanyakazi wake – baada ya kupunguzwa kwa misaada ya USAID, ikiwa ni pamoja na wale waliohusika na uhamasishaji wa jamii, elimu ya afya na kuzuia Ebola.

“Wakati Ebola hii mpya ilipozuka, wafanyakazi hawakuwepo, mikakati ya kukabiliana na hali ya dharura pia haikuwepo,” anasema.

“Kwa ufadhili unaofaa, tungelijipanga mapema na kuanza kusambaza vifaa muhimu kama vile PPE kuanzia siku ya kwanza, lakini tulianza kukabiliana na hali hiyo bila ya kuwa na chochote na kupoteza siku 10.”

Wakosoaji wanaelezea kuvunjwa kwa USAID kama pigo kwa kasi ya kugundua mlipuko wa Ebola na kiwango cha mwitikio, wakisisitiza kwamba shirika la kibinadamu lilikuwa muhimu katika kutoa vifaa, na kufikia watu vijijini.

Marekani inakanusha kwamba kupunguzwa kwa misaada yake kumeathiri juhudi hizo, ikisema kwamba “zinaendana zaidi na zinafaa” chini ya mpango mpya wa dola milioni 270 ambazo imechangia kukabiliana na janga hilo.

Kinachochangia mikataba ya Marekani ni hamu ya utawala ya kuhimiza serikali za kitaifa kutumia pesa zao zaidi kwenye huduma zao za afya – waangalizi wanasema barani Afrika hali imekuwa mbaya zaidi, licha ya kujitolea kwa bara hilo kufanya hivyo mwaka wa 2001.

Marekani imetoa mchango wa dola milioni 270 kukabiliana na mlipuko wa sasa wa Ebola.

Chanzo cha picha, Reuters

Lakini wengine wanaonya kwamba mlipuko wa Ebola umeangazia hatari inayokabili mpango wa pande mbili kwa afya ya kimataifa.

“Makubaliano ya pande mbili hupuuza changamoto za pamoja,” anasema Dkt. Kevin DeCock, mkurugenzi wa zamani katika Vituo vya Kudhibiti Magonjwa vya Marekani (CDC) ambaye alifanya kazi kwa miaka mingi katika mstari wa mbele katika kupambana na magonjwa ya kuambukiza.

“Afya ya kimataifa, kwa ufafanuzi, ni ya kimataifa, inavuka mipaka, haihusishi nchi moja tu. Matatizo ya afya ya kimataifa yanahitaji mbinu za kimataifa, na hakuna nchi inayoweza kujiendesha yenyewe.”

Baadhi ya wachambuzi wa sera za afya na mambo ya nje wametetea kuipa nafasi mkakati mpya wa utawala.

Katika makala ya taasisi ya mawazo ya kihafidhina ya Taasisi ya Biashara ya Marekani, Brett Schaefer na Roger Bate wanakiri hatari ya kujiondoa katika mfumo wa pande nyingi, hasa kujiondoa kutoka kwa WHO.

Lakini huu “sio mwisho wa uongozi wa Marekani katika afya ya kimataifa”, wanaandika. “Ni mwanzo wa jaribio – la kuhakikisha udhibiti unatekelezwa vyema kupitia ushirikishwaji wa masharti, taasisi sambamba na ushirikiano unaotokana na shirika ambalo limejitahidi kujifunza kutokana na makosa.”

Kulichojitokeza kufikia sasa ni kwamba miezi kadhaa baada ya Rubio kutia saini makubaliano ya kwanza ya MOU, utata ungalipo linapokuja suala la kufikiwa kwa makubaliano ya pande mbili barani Afrika.

Tanzania imesaini ushirikiano huo, huku mataifa kadhaa ya Afrika yakisusia mpango huo, kilichobakia ni kusubiri matokeo ya mkakati huu mpya wa afya ya kimataifa ya Markani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *