
Jeshi la Israeli limethibitisha kujeruhiwa kwa wanajeshi wake sita katika nyakati tofauti nchini Lebanon.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wanajeshi wawili walijeruhiwa baada ya kushambuliwa kusini mwa Lebanon Jumapili ya wikendi iliopita.
Maofisa wengine watatu wa IDF walijeruhiwa, mmoja kati yao akijeruhiwa vibaya baada ya ndege isiokuwa na rubani kuanguka karibu na eneo walipokuwa.
Kulingana na taarifa ya jeshi la Israeli, afisa wake mwengine alijeruhiwa katika ajali ya oparesheni za kijeshi na wote waliojeruhiwa wanaendelea kupokea matibabu hospitalini.
Israel ilianzisha tena oparesheni za kijeshi nchini Lebanon baada ya wapiganaji wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran kurusha makombora kaskazini mwa Israeli kujibu mauaji ya kiongozi wa juu wa kiroho wa Iran Ali Khamanei.
Tangu wakati huo, zaidi ya watu Elfu Moja wameuwa katka mashambulio ya Israeli nchini Lebanon kwa mujibu wa Wizara ya afya kwenye taifa hilo.
Israel aidha imesema itaongeza oparesheni zake kusini mwa Lebanon katika kampeni yake dhidi ya wapiganaji wa Hezbollah.