#HABARI: Raia wa Uganda, Fortunate Kyarikunda, amehukumiwa kifungo cha miezi 6 jela baada ya kushindwa kulipa zaidi ya Milioni 14 sawa na Shilingi milioni 9.6 za Kitanzania kwa mwanaume aliyemlipia ada akitarajia ndoa lakini akaachwa.

Mwanaume huyo, mwalimu wa shule ya msingi, alidai alitumia pesa hizo kumsomesha Kyarikunda kwa matumaini ya kumuoa, ndoto ambayo haikutimia.

Mahakama iliamuru alipe fidia, lakini Kyarikunda alishindwa kutekeleza hukumu na hata kupuuza wito wa mahakama mara kadhaa.

Kutokana na kuchelewesha, deni liliongezeka hadi zaidi ya shilingi milioni 14.

Mwishowe, Mahakama ya Rukungiri ikaamuru afungwe hadi miezi 6 au hadi alipie deni lote.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *