Tunaposherehekea miaka 30 ya Advent Construction Ltd, ni wakati wa kutafakari safari yetu ya kuvutia iliyoanzia chini kabisa, tukiongozwa na nia iliyowazi ya kufanya kazi nzuri na kujenga imani kwa muda mrefu kwa wadau wetu, na hamu isiyoisha ya kujikita kwenye ubora na kuaminika kwa chapa yetu.
Wakati tunaanza lengo letu lilikuwa wazi ya kwamba tunataka kutimiza ahadi zetu na kujenga mahusiano endelevu. Misingi hiyo haijabadilika mpaka leo hii, na haitabadilika, licha ya mabadiliko mengine muhimu tuliyoyakubali katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita.
Ahadi yetu ya kuendelea kutekeleza miradi yenye ubora wa hali ya juu ndiyo inayotutofautisha sokoni, na ni msingi ambao umesababisha Advent kutambulika mara kwa mara kama kampuni ya kipekee ikilinganishwa na kampuni nyingine. Kila mradi uliokamilika ni ushuhuda wa heshima wa ahadi hii.
Tunapotazama tulipotoka katika safari hii ya kusisimua, licha ya mara kadhaa kukabiliana na changamoto, ni vyema kushukuru wale wote ambao wametushika mkono, kutuongoza, kutufunza, na muhimu zaidi, kutuamini na kutukabidhi miradi yao mikubwa zaidi. Kwa niaba ya Advent na yangu binafsi, nina fahari kutambua michango ya dhati ya wale wote walioshiriki katika safari yetu.
Mradi wa upanuzi wa kiwanda cha sukari ghafi cha TCH 420 cha Kilombero.
Nchi yetu sasa ipo katika mwelekeo unaotia moyo ikichagizwa na fursa nyingi za ukuaji na maendeleo, na Advent inakusudia kuwa mstari wa mbele katika kutumia fursa hizi kwa maendeleo ya watu wetu na Taifa.
Tunayo matarajio makubwa kwa siku za usoni, huku hatma ya Advent ikiwa kwenye mikono salama ya vijana wenye ujuzi wa kipekee, ambao wanaoamini kikamilifu katika misingi yetu ya uasisi wa kampuni ya kufanya kazi kwa moyo wa dhati, ubora, na uaminifu.
Pia tunaamini bado tutaendelea kushikwa mkono na marafiki wetu wote na wale wanaotutakia mema, huku tukikaribisha wale wote watakaokuwa sehemu ya safari yetu katika siku zijazo.
Miaka 30 ya uongozi, mafunzo na safari ya karne mpya ya Advent Construction
Mkurugenzi Mtendaji wa Advent Construction, Dhruv Jog.
Wakati Advent Construction Ltd ikiadhimisha miaka 30 ya mafanikio, Mkurugenzi Mtendaji wake, Dhruv Jog anatupitisha katika safari iliyojengwa juu ya ustahimilivu, kujifunza na maono ya muda mrefu.
Kutoka kuwa kampuni iliyoanzia chini kabisa hadi kuwa moja ya kampuni zinazoheshimika zaidi za ujenzi nchini, simulizi ya Advent inawakilisha watu, dira na mafanikio ya kudumu.
Na hii ni sehemu ya mahojiano na mwandishi makala hii:-
Swali: Maadhimisho ya miaka 30 yana maana gani kwako binafsi na kwa mustakabali wa Advent?
Jibu: Miaka 30 ni hatua kubwa sana. Kuna wakati naitazama kampuni kama binadamu, huanza kwa kujifunza, kama mtoto anavyojifunza kutembea. Miaka 20 ni hatua ya ukuaji, lakini miaka 30 ni ukomavu.
Hapo unakuwa umejifunza masomo mengi muhimu. Kampuni ikifikia miaka 30, ina nafasi kubwa ya kufikisha miaka 100. Huu ni uthibitisho wa uimara wetu. Mafanikio haya yanatokana na uthabiti na uvumilivu, mambo ambayo hayawezi kuharakishwa.
Umeitumikia kampuni kwa takriban miaka 20. Umejifunza nini kama kiongozi?
Nimebahatika kukulia ndani ya kampuni, nikishika nafasi mbalimbali hadi kufikia kuwa mkurugenzi mtendaji. Kila siku najifunza jambo jipya. Biashara hubadilika kila siku. Siamini kuwa kuna mtu anayejua kila kitu. Mtazamo wa kujifunza kila siku ndio unaotusukuma kusonga mbele. Kwa kweli, nahisi kama ndo kwanza nimeianza hii safari.
Swali: Ni hatua zipi muhimu zimeijenga Advent kuwa ilivyo leo?
Jibu: Mafanikio ya kifedha ni kipimo kimojawapo. Tumekua kutoka kuingiza mamilioni hadi mabilioni ya mauzo kwa mwaka. Lakini kwangu, mafanikio yasiyo ya kifedha ni muhimu zaidi. Kupata cheti cha ithibati cha ISO mwaka 2012 kama kampuni ya kwanza ya ujenzi ya Kitanzania ni jambo la kujivunia.
Jengo la Faykat Tower la biashara na ofisi lililopo Kinondoni, jijini Dar es Saalam.
Vyeti havileti fedha moja kwa moja, lakini vinaweka mifumo imara ya kudumu. Pia, mwaka 2019 tulitambuliwa na Soko la Hisa la London kama “Kampuni Yenye Ushawishi Afrika,” jambo lililothibitisha kuwa kampuni ya kizawa inaweza kufikia viwango vya kimataifa.
Swali: Advent inachangiaje katika uendelevu na miundombinu ya kisasa?
Jibu: Uendelevu huanza kwenye usanifu. Miundo ya sasa ni rafiki zaidi kwa mazingira. Ingawa gharama zake ni kubwa, tunajitahidi kupunguza athari kwa mazingira. Pia tunaweka mifumo ya kisasa ya kusimamia majengo baada ya ujenzi ikichagizwa na ukuaji wa teknolojia.
Swali: Kampuni imechangiaje maendeleo ya Taifa?
Jibu: Kazi zetu zinagusa sekta nyingi kuanzia viwanda, miundombinu, maji na nyinginezo. Tumejenga viwanda vya mwanzo, miradi ya umwagiliaji, viwanja vya ndege na miradi ya madini. Tunakua pamoja na mahitaji ya nchi. Kiwanda cha kwanza cha jasi na mchele kimejengwa nasi.
Swali: Je, mnarudisha kwa jamii?
Jibu: Ndiyo. Tunafadhili masomo ya wanafunzi bora wa uhandisi na ukadiriaji majengo pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Tunajenga wataalamu wa baadaye, si miradi tu.
Swali: Mustakabali ukoje?
Jibu: Kuna fursa kubwa, hususan kuongeza ushiriki wa wazawa katika sekta ya ujenzi. Kwa msaada sahihi, kampuni za Kitanzania zinaweza kufanya zaidi. Kesho yetu inaonekana kuwa bado nzuri na tuko tayari.
Ujumbe wa Mhe. Waziri wa Maji
Waziri wa Maji wa Tanzania, Mhe. Jumaa Aweso.
Nikiwa kama Waziri mwenye dhamana ya sekta ya maji nikiri bayana ya kwamba ninafarijika sana na najisikia fahari kuona wakandarasi wazawa wakitekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati ya sekta ya maji.
Wizara ya Maji imeendelea kufungua milango kwao na kutenegeneza mazingira mazuri ya kufanya kazi na kuwaamini.
Ninajivunia kazi inayofanywa na Advent katika sekta yetu, ninathamini mchango wao katika kuibeba ajenda ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumtua mama ndoo kichwani.
Ninaamini msingi bora wa mafanikio katika sekta yetu ni kuwa na wakandarasi wanaofanya kazi kwa moyo, ufanisi, kazi ya uhakika na kwa wakati, nimekagua mara nyingi kazi zinazotekelezwa na Advent na ninaridhishwa na kazi nzuri wakati huohuo nikiendelea kushauri na kutoa ushirikiano wa dhati.
Mradi wa mtambo wa matibabu ya maji jijini Tanga.
Hongera sana kwa miaka 30 ya mafaniko na mageuzi makubwa. Sekta ya maji tunajivunia miradi mliokamilisha katika kipindi hiki na tunawatakia kila lakheri kumalizia miradi mliopata fursa kushirikiana nasi mkaikamilishe kwa wakati na viwango.
Ujumbe wa Mteja
Mwaka 2017, kampuni ya Knauf ilianzisha kiwanda kipya cha uzalishaji wa mbao za jasi (gypsum boards) nchini kwa kushirikiana na Advent kama mshirika wa kuaminika.
Meneja Mradi Knauf Engineering GmbH, Burkard Frey.
Mradi huo ulikuwa na mahitaji makubwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mnara wa kiwanda cha jasi wenye urefu wa mita 30, jengo la uzalishaji lenye ukubwa wa mita za mraba 5,000, maghala yenye ukubwa wa mita za mraba 8,000, pamoja na ofisi, maeneo ya kijamii, maabara, na kazi za nje zikiwemo barabara.
Kati ya wazabuni wengi, Advent haikuwasilisha tu pendekezo shindani, bali pia ilivutia wengi kutokana na mbinu yake ya kiufundi iliyobuniwa kwa umakini mkubwa, jambo ambalo ni muhimu sana kwa mikataba inayohusisha usanifu na ujenzi.
Licha ya changamoto za hali ya udongo, vipindi vya hali mbaya ya hewa, pamoja na viwango vya juu vya ubora vilivyowekwa na Knauf, Advent ilitekeleza mradi huo kwa weledi mkubwa na kwa kurkidhi matarajio yetu.
Mwaka 2022, Knauf iliamua kupanua eneo hilo la kiwanda na kuongeza takriban mara tatu ya uwezo wake wa uzalishaji. Advent ilishinda tena zabuni ya kazi za ujenzi na kwa mara nyingine ikaonyesha utendaji wenye ubora wa hali ya juu.
Ushirikiano ulikuwa wenye ufanisi, uliozingatia utatuzi wa changamoto, na uliotawaliwa na mawasiliano ya wazi, jambo lililowezesha mradi kusonga mbele kwa haraka na kiwanda kukamilika kwa mafanikio.
Kiwanda cha uzalishaji mbao za jasi (gypsum boards) kilichopo Mkuranga, mkoani Pwani.
Kama meneja wa mradi, ninathamini sana utaalamu mkubwa wa kiufundi wa Advent, uaminifu wake, pamoja na dhamira yake ya kufanikisha kazi. Kama ilivyo kwa Knauf, Advent pia ni kampuni inayoendeshwa na familia yenye muundo wa uongozi thabiti, hali inayowezesha kufanya maamuzi kwa haraka na kutoa majibu ya haraka yanapotokea mabadiliko au changamoto.
Tunawashukuru Advent kwa kazi yao bora na tunatarajia kushirikiana nao tena katika miradi ijayo.
Advent Construction ilivyojijengea heshima kupitia ubora, usalama na uongezaji thamani katika sekta ya ujenzi nchini
Mkadiria Majenzi wa Kampuni ya Advent Construction, Editha Mujuni.
Kwa zaidi ya miongo mitatu, Advent Construction imejijengea sifa kama moja ya kampuni za ujenzi zilizo imara, zinazoheshimika na za kuaminika zaidi nchini, ikiongozwa na dhana kwamba ubora, usalama na ufanisi wa gharama lazima viende sambamba ili kuhakikisha utekelezaji wenye mafanikio wa miradi.
Mafanikio haya ya muda mrefu yanatokana na mbinu thabiti na ya kimfumo inayosimamia kila hatua ya ujenzi, kuanzia upangaji wa awali hadi makabidhiano ya mwisho, huku msisitizo mkubwa ukiwekwa katika udhibiti makini wa gharama na ununuzi wenye ufanisi.
Muendelezo wa ubora huwezeshwa kupitia uzingatiaji vielelezo na masharti ya kimkataba pamoja na kujumuisha viwango vinavyosimamia sekta ya ujenzi katika shughuli za kila siku. Ufuatiliaji endelevu wa utendaji husaidia kubaini hatari mapema, wakati ushirikiano wa wazi na wateja pamoja na wadau huimarisha uwajibikaji na kuongeza thamani ya miradi.
Kampuni imefanikiwa kuweka uwiano sawa baina ya ufanisi wa gharama na viwango vya juu vya ubora na usalama kupitia mipango makini, utabiri wa gharama wa mapema na uboreshaji wa thamani wa sekta ya uhandisi. Ununuzi wa kimkakati na kuwa na mtandao wa wasambazaji wa uhakika hupunguza hatari, wakati huo huo, uthibiti wa gharama husaidia miradi kutekelezwa ndani ya bajeti iliyopangwa.
Jengo la Mlimani Plaza (SkyCity) lililopo Mlalakuwa, jijini Dar es Salaam.
Uwezo wa Advent unaonekana katika miradi mbalimbali, ikiwemo ile maendeleo ya Mlimani Plaza (SkyCity) jijini Dar es Salaam, miradi ya viwandani Mkuranga na Morogoro, pamoja na miradi ya miundombinu ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga.
Kupitia utawala bora, ubunifu na mtazamo wa thamani ya muda mrefu, Advent inaendelea kutekeleza miradi yenye athari chanya huku ikijenga imani ya kudumu.
Mradi wa Umwagiliaji wa Lyamalagwa uliopo mkoani Tabora.