trump

Chanzo cha picha, EPA

Rais Donald Trump amewaambia waandishi wa habari kwamba
Marekani “itaondoka[Iran] hivi karibuni” na hatua za kijeshi za nchi hiyo zitakomeshwa
ndani ya “wiki mbili au tatu”

Anasema Marekani imefikia malengo iliyojiwekea
kabla ya kuanza kwa mashambulizi ya anga dhidi ya Iran mwezi uliyopita kwa ushirikiano na Israel. Ameongeza
kuwa lengo la kuizuia Iran kuwa na uwezo wa kuunda silaha za nyuklia limefikiwa
na sasa Marekani “inamaliza kazi”

Trump pia anasema Marekani sasa inatawala anga la Iran na pia imepata
mabadiliko ya utawala kufuatia mauaji ya viongozi wakuu wa kisiasa na kijeshi.
Aliwataja viongozi hao wapya mjini Tehran kama “walio na misimamo
mikali” na “waadilifu zaidi” ikilinganishwa na watangulizi wao.

Trump pia anasema viongozi wa Iran “wanaomba
kufanya makubaliano” na Marekani ili kumaliza vita, madai ambayo hapo
awali yalipingwa na Iran.

Anaongeza kuwa vita vinaweza kumalizika bila
makubaliano kati ya pande hizo mbili.

Kuhusu athari za vita hasa kupanda kwa bei ya
mafuta, rais Trump anasema bei itashuka mara tu Marekani itakapomaliza hatua
zake za kijeshi.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *