
Nchini Senegal, Rais Bassirou Diomaye Faye ametia saini sheria mpya inayopambana na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Sheria hii mpya inaongezeka adhabu mara mbili kwa watu watakaopatikana kujihusha na vitendo hivyo ambavyo ni marufuku nchini Senegal.
Sheria hiyo ambayo ilipata uungwaji mkubwa wa wabunge, inaeleza kuwa yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, atafungwa jela miaka 10 kutoka miaka mitano.
Wale watakaobainika kupigia kampeni vitendo hivyo kwa kutoa fedha, watafungwa jela miaka saba kutoka miaka mitatu.
Sheria hii inaanza kufanya kazi baada ya mwezi Februari, wanaume zaidi ya 10 waliokuwa wanahusishwa na vitendo hivyo kukamatwa na polisi.
Kabla ya hatua hii, maafisa wa serikali na wabunge wamekuwa katika shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa dini na wananchi wa kawaida, kutaka sheria kali zaidi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia, wanaosema, vinalazimishiwa kwa raia wa taifa kutoka mataifa ya nje ili kuharibu maadili ya Senegal