
Nchini Senegal, rais Bassirou Diomaye Faye, leo anaadhimisha miaka miwili tangu aliposhika madaraka katika nchi hiyo, wakati huu akiendelea kukabiliwa na shinikiza za kutekeleza ahadi alizotoa kwa raia wa nchi hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais Faye mwenye umri wa miaka 43, aliingia madarakani na kuandikisha historia ya kuwa rais mwenye umri mdogo kwenye historia ya uongozi nchini humo.
Alipigiwa kura, baada ya kuchukua nafasi ya mshirika wake wa karibu, Waziri Mkuu wa sasa Ousmane Sonko, ambaye alikuwa awe mgombea urais, lakini akazuiwa baada ya kufungwa jela.
Miaka miwili baadaye, kuna mashaka kuwa ushirikiano wake na Sonko umeanza kuyumba baada ya wawili hao kuonekana kuanza kujipanga upya kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2029, kila mmoja akijaribu kuonesha ushawishi kwenye chama tawala Pastef.
Wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa hatua ya rais Faye na Waziri Mkuu Sonko, kupambania ushawishi ndani chama hicho, unaendelea kuwagawa na kuathiri utekelezwaji wa ahadi ya maendeleo kwa wananchi wa Senegal, na ni ishara kuwa wawili hao kila mmoja anajipanga kuwania urais wa wakati wa uchaguzi ujao.