
Nchini Rwanda, kundi la watu 214 wanaohusishwa na makundi ya waasi, ikiwa ni pamoja na FDLR kulingana na mamlaka, wamerejeshwa katika maisha ya kiraia baada ya miezi kadhaa katika kituo walikkokuwa wamekusantwa kwa ajili ya kupewa maadili ya namna ya kuishi upya na raia. Miongoni mwao ni wapiganaji pamoja na raia wanaohusishwa na makundi haya.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud
Chini ya mahema kulikokuwa kukifanyika sherehe, Kazungu Kabahizi anasherehekea mwisho wa zoezi la kurejeshwa kwake katika maish ya kiraia. Baada ya kuondoka Rwanda mwaka wa 1994 na kupigana katika kundi lenye silaha kama FDLR, sajenti huyo anasema aliamua kukimbia mwaka jana, baada ya mapigano makali dhidi ya M23.
“Ni wakati huo ndipo nilipogundua uzito wa hali hiyo: wenzangu wengi waliuawa, wengine walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hadi Beni kwa matibabu.” “Nilianza kufikiria kurudi nyumbani, lakini jaribio lolote la kutoroka lilikuwa hatari sana, kwa sababu ikiwa mpango wetu ungegunduliwa, tungeliweza kuuawa,” anasimulia.
Kwa miezi kadhaa, katika kituo cha Mutobo, wanajeshi waliorejeshwa katika maisha ya kiraia walishiriki katika kozi za elimu ya uraia na ujumuishaji upya. Baada ya miongo kadhaa nchini DRC, Kazungu Kabahizi aliungana tena na ndugu zake waliokuwa wamebaki Rwanda. “Tuliwasiliana kwa simu hata nilipokuwa bado huko (nchini DRC); walinitumia ujumbe. Ugumu pekee ulikuwa kujua jinsi ya kurudi Rwanda,” anasema.
“Lazima tuwaondoe shaka”
Kwa jumla, Tume ya kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia (RDRC) inadai kuwa imewasaidia zaidi ya watu 12,000 tangu mwaka 2001. Kuvunjwa kwa FDLR, kundi lenye silaha ambalo awali liliundwa na wahalifu wa zamani wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, lililokuwa na makao yake kwa miaka 30 mashariki mwa DRC, ni mojawapo ya masuala ya usalama yaliyoshughulikiwa na Kigali katika Makubaliano ya Washington.
Hii ni kazi ngumu, pia kwa jamii zinazowapokea, anathibitisha mwenyekiti wa tume hiyo, Valérie Nyirahabineza. “Lazima kabisa tuwaandae sio familia tu, bali pia jamii kwa ujumla, kuwakubali. Tusiwaone kama wapiganaji. Watakapokubali kuweka silaha zao chini, lazima tuwaondoe shaka,” anaamini.
Mwishoni mwa kurejeshwa kwaokatika maisha ya kiraia, wapiganaji wa zamani wanarudi kwenye vijiji vyao vya familia, huku zaidi ya nusu ya kundi hilo wakirejeshwa katika maisha ya kiraia tena wiki hii katika wilaya ya Rubavu inayopakana na Goma.