Serikali kupitia Wizara ya Afya imetangaza mkakati mpya wa kuimarisha afya za wananchi kwa kuhakikisha elimu ya afya inawafikia wananchi moja kwa moja kupitia huduma ya nyumba kwa nyumba.
Akizungumza leo tarehe 2 Aprili, 2026 jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Waziri wa Afya na Wadau wa Sekta ya Dawa, Mkurugenzi wa Huduma za Uhamasishaji wa Afya (Elimu ya Afya kwa Umma), Dkt. Rahma Hingora amesema Serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anapata elimu sahihi ya afya bila kujali mahali alipo.
Amesema kupitia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii(CHW),wananchi watapatiwa elimu elimu ya kina na inayoendana na maisha yao ya kila siku,ikihusisha itahusisha matumizi ya vyakula vya asili ,kinga dhidi ya magonjwa, pamoja na kuhamasisha mtindo bora wa maisha.
“Tunataka kuona elimu ya afya inamfikia mwananchi moja kwa moja nyumbani kwake. Hii itasaidia kuongeza uelewa, kubadili tabia hatarishi, na kuimarisha kinga ya jamii dhidi ya magonjwa, tutaelemisha upatikanaji wa dawa sahihi na maeneo sahihi, matumizi sahihi na madhara ya kutofuata utaratibu sahihi wa matumizi ya dawa ” amesema Dkt. Hingora.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *