Madaraja mawili mapya yaliyolengwa na jeshi la Israel yako katika eneo muhimu linalounganisha Bonde la Bekaa mashariki na kusini mwa Lebanon. Yanadhibiti ufikiaji kati ya mwambao wa ziwa kubwa zaidi nchini na njia zinazoelekea kusini mwa Lebanon, ambapo Israel imekuwa ikijaribu kusonga mbele kwa karibu mwezi mmoja. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa kuharibu madaraja haya, jeshi la Israel linalenga kukata njia zinazotumiwa kwa ajili ya misaada ya kijeshi ya Hezbollah, ambazo utumiwa kwa kusafirisha vifaa vya ziada na vifaa vya kijeshi kutoka ngome zake katika Bonde la Bekaa hadi kwenye mstari wa mbele.

Jeshi la Israel liliandamana na vitisho vyake vya kuharibu madaraja hayo mawili kwa kuwasihi wakazi wa eneo hilo kuhama vijiji vyao na kuelekea kaskazini.

Tangu mwanzo wa vita, jeshi la anga la Israel limeharibu madaraja saba yanayozunguka Mto Litani na kuelekea kusini mwa Lebanon. Miongoni mwao ni Daraja la Qasmiyé, lililoko kwenye barabara kuu ya pwani inayoelekea mji wa bandari wa kale wa Tiro.

Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza kwa vitisho kuelekezwa katika eneo la Bonde la Bekaa, kuonyesha nia ya kutenga zaidi Kusini, ambapo tayari watu wameuhama mji huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *