Watu wanane wa familia moja wamefariki katika jimbo la Kabul kufuatia tetemeko la ardhi lililosikika kote Afghanistan Ijumaa jioni, Aprili 3, Wizara ya Afya ya Afghanistan iliripoti siku moja baadaye.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.8 katika kipimo cha Richter  lilitokea saa 2:42 usiku kwa saa za huko kaskazini mashariki mwa Afghanistan kwa kina cha kilomita 186.4, kulingana na shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani (USGS). 

Angalau watu wanane wamefariki kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.8 katika kipimo cha Richter lililotokea kaskazini mwa Afghanistan Ijumaa jioni, amesema Mohammad Yousuf Hammad, msemaji wa Mamlaka ya kitaifa ya Usimamizi wa Maafa.

Nyumba moja katika jimbo la Kabul imeanguka kutokana na tetemeko hilo, na kuwaua wakazi wanane na kumjeruhi mtoto, amebainisha.

Kitovu cha tetemeko hilo kilionekana na Taasisi hiyo kilomita 35 kusini mwa Jorm, katika jimbo la Badakhshan, lakini tetemeko hilo lilisikika katika majimbo mengi ya Afghanistan, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Kabul, kulingana na waandishi wa habari wa AFP.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *