
Ripoti zinaonyesha
kuwa Marekani na Iran zinashindana kwa kasi kumtafuta rubani wa pili wa ndege ya
kivita ya Marekani iliyodunguliwa katika eneo la kusini mwa Iran.
Operesheni hiyo
imekuwa ya dharura huku pande zote zikijaribu kumfikia mhudumu huyo kabla ya
mwingine.
Hapo awali, uchunguzi
wa BBC Verify ulithibitisha video iliyokuwa ikisambaa mtandaoni ikionyesha kile
kinachoonekana kuwa ndege ya Marekani ikifuatana na helikopta mbili, zikifanya
operesheni ya utafutaji na uokoaji.
Video hiyo
ilithibitishwa kushambuliwa katika jimbo la Khuzestan, karibu na daraja juu ya
mto Karun.
Video hiyo
imechunguzwa ili kuthibitisha kuwa ni ya hivi karibuni na pia kuangaliwa kama
ina dalili zozote za kutengenezwa kwa teknolojia ya AI, lakini hakuna ushahidi
uliopatikana unaoonyesha udanganyifu.
Hii inaongeza uzito wa
taarifa kuwa operesheni hiyo ni halisi.
Kwa mujibu wa ripoti
kutoka Marekani, zikimnukuu maafisa wasiotambulishwa majina, operesheni hiyo
imefanikiwa kumwokoa mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo, lakini juhudi bado
zinaendelea kumtafuta rubani wa pili ambaye hajapatikana.
Wataalamu wa masuala
ya kijeshi wanaeleza kuwa operesheni kama hizi ni hatari sana na zinahitaji kufanyika
kwa haraka zaidi.
James Jeffrey,
mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani, amesema kuwa hii ni miongoni mwa oparesheni hatari zaidi za kijeshi, kwani hujumuisha helikopta, ndege za kuongeza mafuta
angani, na ndege za kulinda eneo hilo.
Kwa upande mwingine, mhudumu na rubani wa ndege walioanguka huwa wamefunzwa kukabiliana na hali kama hizi.
Kipaumbele chao kikuu
ni kubaki hai na kuepuka kukamatwa, ikiwa ni pamoja na kujificha na kuondoka
haraka katika eneo walipoangukia.
Aidha, hupatiwa
mafunzo ya mbinu za kuishi mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kupata
chakula na maji au kuhimili bila hivyo kwa muda.
Hii huwasaidia
kuongeza nafasi ya kuokolewa kabla hawajapatikana na maadui.
Unaweza kusoma pia: