Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa waliohusika na mauaji katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Kilosa Mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa Matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Adrew Kantimbo amesema tukio la kwanza limetokea Jioni ya April 4 mwaka huu katika kitongoji cha Mkukuzi chin katika kijiji cha Nyambeni kilochopo Kata na Tarafa ya Ulaya Wilayani Kilosa.

Ambapo katika tukio hilo Janeth Mazengo umri wake miaka 52 mkulima ambae aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali Sehem Mbalimbali za mwili wake na mumewe aitwae Amos Zakaria kutoka na wivu wa kimapenzi.

Mtuhumiwa huyo amelazwa katika kituo cha afya Ulaya baada ya kufanya jaribio la kunywa sumu baada ya kufanya mauaji hayo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *