Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Saidi Miraji amesema Hayati Abeid Amani Karume alikuwa kiongozi mwenye falsafa ya kuunganisha jamii na kupunguza matabaka.

Ameeleza kuwa moja ya mbinu alizotumia ni kuhimiza ndoa kati ya makabila tofauti, hatua iliyosaidia kujenga mshikamano na kuondoa ubaguzi wa kijamii.

Aidha, Miraji ameongeza kuwa Karume alithamini Muungano kwa kuzingatia utawala wa serikali mbili, jambo lililosaidia kuimarisha umoja na utulivu wa taifa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *