#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi, ametoa zawadi ya gari jipya kwa kila mchezaji na mwanachama wa benchi la ufundi la timu ya taifa, “The Leopards”. Hatua hii imekuja kama pongezi baada ya timu hiyo kufanikiwa kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026 zitakazofanyika nchini Marekani, Canada, na Mexico.

Mafanikio haya yameandika historia mpya nchini humo kwani ni mara ya kwanza kwa DR Congo kufuzu michuano hiyo mikubwa baada ya kusubiri kwa miaka 52. Mara ya mwisho kwa nchi hiyo (wakati huo ikijulikana kama Zaire) kushiriki Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1974 nchini Ujerumani Magharibi, ambapo waliondolewa katika hatua ya makundi.

Rais Tshisekedi amewapongeza wachezaji kwa juhudi na nidhamu waliyoonyesha uwanjani, akisema kuwa wameiletea nchi heshima kubwa na kuwapa furaha mamilioni ya Wakongo. Zawadi hizo za magari ya kifahari zimetolewa ili kuwatia moyo wachezaji kuelekea fainali hizo ambapo DR Congo inatarajiwa kuipeperusha vyema bendera ya Afrika.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *