Ikiwa ni zaidi ya saa 24 tangu Rais wa Marekani Donald Trump atangaze kusitisha mapigano kwa wiki mbili nchini Iran, jambo ambalo Israel, Iran na wapatanishi wa Pakistan walilithibitisha, lakini tayari makubaliano ya amani yanaonyesha kuyumba.
Hatua hiyo ni baada ya Israel kuanzisha wimbi la mashambulizi nchini Lebanon, na kuua watu wasiopungua 182.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea mashambulizi hayo kama pigo kubwa kwa Hezbollah tangu kuanza kwa vita, akisema Israel itaanza tena kupigana na Iran kukiwa na haja ya kufanya hivyo.
Wakati huo huo, Iran imesema ikiwa mashambulizi nchini Lebanon hayatakoma mara moja huenda yakachochea hatua kuchukuliwa.
Jumamosi wiki hii, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance atashiriki katika mazungumzo na Iran mjini Islamabad, Pakistan.
Jambo la msingi katika mazungumzo hayo ni kuhusu usafiri wa meli za mafuta katika Mlango-Bahari wa Hormuz, njia ya baharini katika Ghuba ya Uajemi ambayo ni muhimu kwa usambazaji wa mafuta duniani.
Iran imetishia kuzishambulia meli na kuzharibiwa endapo zitapita bila ruhusa.
#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)