
Kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 uliofanyika mwezi uliopita katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Anold Kayanda wa Idhaa hii aliketi na Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya ili kusikia ni kwa namna gani Kenya inapiga hatua katika Lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.