Serikali yajenga Km 1,759 za barabara mipakaniSerikali yajenga Km 1,759 za barabara mipakani

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, amesema Serikali inaendelea kujenga barabara za usalama mpakani kwa kiwango cha changarawe ili kurahisisha shughuli za vyombo vya ulinzi na usalama katika doria mipakani.

Akijibu swali bungeni jijini Dodoma, Kasekenya amesema hadi sasa Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imefanikiwa kujenga jumla ya kilometa 1,759 za barabara kwa kiwango hicho katika mikoa ya mipakani. Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga sehemu zilizobaki kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. SOMA: Maelekezo ya utu ujenzi wa barabara yazingatiwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *