Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) leo limeonya kuwa vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati vinaweza kusukuma “sehemu kubwa ya wananchi wa Iran katika umaskini wa kupindukia huku maisha ya kila siku na shughuli za kiuchumi zikivurugika.”

Katika ripoti yake UNDP imeanisha mambo Matano muhimu yanaypdhihirika kuwa taifa hilo liko mashakani sio tu katika masuala ya usalama bali pia katika maendeleo na hasa ya kiuchumi.

Viwanja vya Hospitali ya Al Shifa mjini Gaza. Ili kusaidia juhudi za uokoaji, UNDP inatoa ajira za dharura katika huduma za afya, elimu na sekta binafsi.

© UNDP PAPP

Mfanyakazi wa UNDP akikagua uharibifu katika Hospitali ya Al-Shifa huko Gaza.

Mambo matano muhimu kutoka ripoti ya UNDP

• Kiwango cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) ya Iran kinaweza kushuka kwa hadi pointi 0.56, kikifuta zaidi ya mwaka mmoja wa maendeleo.
• Kupanda kwa bei ya chakula ni changamoto kubwa, huku kaya zenye kipato cha chini tayari zikitumia karibu nusu ya mapato yao kununua chakula.
• Kuvurugika kwa uagizaji wa bidhaa na mishtuko ya bei kunatarajiwa kuzidisha hali mbaya ya maisha, hasa kwa makundi yaliyo hatarini.
• Biashara ndogo ndogo na wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi zinakabiliwa na upotevu mkubwa wa mapato, hali itakayogusa jamii kwa kiwango kikubwa
• Misaada ya kibinadamu na mifumo lengwa ya ulinzi wa hifadhi ya jamii itakuwa muhimu kupunguza ongezeko la umaskini.

Makumi ya mamilioni wako hatarini kuingia kwenye umaskini: UNDP

UNDP pia imeonya kuwa makumi ya mamilioni ya watu duniani wanaweza kuingia katika umaskini kutokana na vita vya Mashariki ya Kati.

Athari mbaya zaidi zinajitokeza katika nchi zilizoathiriwa moja kwa moja na mgogoro huo pamoja na zile zinazotegemea nishati ya kuagiza kutoka nje.

Hata hivyo, ripoti yake mpya inaonyesha madhara makubwa ya muda mrefu kwa nchi maskini zilizo mbali na mapigano.

“Nchi katika ukanda wa Ghuba, Asia, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Nchi Ndogo Zinazoendelea za Visiwa ziko katika ya kipekee,” imeeleza taarifa hiyo.

Tathmini mbaya zaidi ya athari za kiuchumi inaonesha kuwa watu milioni 32 zaidi wanaweza kusukumwa katika umaskini katika nchi 162.

Wajitolea wenye mitandao ya nywele na masks hutoa chakula cha moto kutoka kwenye bakuli kubwa kwa familia za wakimbizi katika kituo cha jamii nchini Lebanon, kama sehemu ya juhudi za misaada ya Shirika la Chakula Duniani (WFP).

© WFP/Marco Frattini

Chakula cha moto kinagawanywa kwa familia za wakimbizi huko Tripoli, Lebanon.

Lebanon: Mhudumu wa dharura aua wakati wa operesheni ya kibinadamu

Vita hivyo vinavyoendelea Mashariki ya Kati kila uchao vinakatilimaisha ya watu wakiwemo wahudumu wa misaada ya kibinadamu.

Afisa mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia kuuawa kwa mhudumu wa kibinadamu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Lebanon wakati wa operesheni kusini mwa nchi hiyo jana Jumapili.

Imran Riza amesema “amehuzunishwa sana na kifo hicho, akitoa pole kwa familia na wahudumu wenzake na kusisitiza kuwa wahudumu wa huduma ya kwanza lazima walindwe wakati wote.”

Kwa mujibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Lebanon, timu hiyo ilishambuliwa moja kwa moja na ndege isiyo na rubani au droni ya Israel ilipokuwa ikijibu tukio karibu na Beit Yahoun, ambapo mhudumu mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa.

UNICEF: Masha ya watoto yako hatarini

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeonya kuwa watoto nchini Lebanon wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi huku mapigano yakiongezeka, yakisababisha vifo, watu kufurushwa na kuvurugika kwa huduma muhimu.

Zaidi ya watu 2,000 wameuawa na wengine zaidi ya 6,500 kujeruhiwa tangu mapema Machi, kwa mujibu wa mamlaka za afya, huku tarehe 8 Aprili ikiwa siku yenye vifo vingi zaidi.

Watoto wasiopungua 33 waliuawa na zaidi ya 150 kujeruhiwa ndani ya siku moja.

Mwanamume anayebeba mtoto amesimama nje ya hema ya bluu iliyowekwa ndani ya jengo la saruji, ambalo linatumiwa kama makao kwa familia zilizohamishwa mjini Beirut, Lebanon.

© UNICEF/Fouad Choufany

Familia waliofurushwa makazi yao wamehifadhiwa katika makao ya muda yaliyoanzishwa katika Sports City huko Beirut, Lebanon.

Ufurushwaji wa watu waongezeka

Zaidi ya watu milioni 1.1 wamekimbia makazi yao, wakiwemo takriban watoto 390,000, wengi wao wakikabiliwa na kuhama mara kwa mara, makazi yenye msongamano na ukosefu wa huduma za afya, elimu na maji safi.

UNICEF inasema ongezeko hilo linaongeza hatari kwa watoto, ikiwa ni pamoja na kutengana na familia, msongo wa mawazo na kuathiriwa na magonjwa katika mazingira yenye msongamano.

Uhaba wa fedha watishia misaada ya kibinadamu

Licha ya vikwazo vikubwa vya kufikia maeneo yaliyoathirika, UNICEF imefanikiwa kuwafikia takriban watu 100,000 katika maeneo hatarishi kwa msaada wa kuokoa maisha na pia kutoa vifaa vya elimu na burudani kwa maelfu ya watoto.

Hata hivyo, shirika hilo linaonya kuwa pengo la ufadhili la karibu asilimia 75 linaweza kuvuruga huduma muhimu huku mahitaji ya kibinadamu yakiendelea kuongezeka.

WHO: Wahudumu wa afya walengwa wa mashambulizi

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa  Duniani (WHO) limekumbusha kuwa wahudumu wa afya na waokoaji wanakabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya kulengwa nchini Lebanonkufuatia vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa wahudumu 57 wa afya wameuawa na angalau 158 kujeruhiwa tangu tarehe 2 Machi, wakati mashambulizi ya roketi ya Hezbollah dhidi ya Israel yalipochochea mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Abdinasir Abubakar, Mwakilishi wa WHO nchini Lebanon, akizungumza na UN News wiki iliyopita alisema  “Unapowaua wahudumu wa afya na waokoaji, pamoja na magari ya wagonjwa matokeo yake ni kwamba hakutakuwa na watu wa kuwasaidia waliojeruhiwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *