Mtafiti mwandamizi wa Kituo cha Utafiti wa Asia Magharibi katika Taasisi ya Uchumi wa Dunia na Mahusiano ya Kimataifa ya Primakov ya Russia anaamini kuwa: Moja ya vipengele muhimu zaidi katika urithi wa kimkakati wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kuanzishwa kwa mfumo wa kisiasa unaoweza kustahimili shinikizo la nje.

Mtafiti mwandamizi Evdokiya Dobrova kutoka Kituo cha Utafiti wa Asia Magharibi cha Taasisi ya Uchumi wa Dunia na Mahusiano ya Kimataifa ya Primakov ya Russia amesema hayo katikaa mahojiano na shirika la habari IRNA siku ya Jumamosi na kueleza kwamba,

Katika kipindi cha miongo kadhaa ya uongozi wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Iran haikuendeleza tu uwezo wake wa kijeshi, bali pia imejenga mfumo mpana wa kiutawala unaoweza kuhakikisha uendeshaji wa serikali hata katika mazingira ya mizozo au hali ngumu.

Alieleza kuwa: Mfumo wa kipekee wa mgawanyo wa madaraka nchini Iran, uliowekwa kwa busara chini ya uongozi wa kiongozi shahidi, ulipunguza kwa kiasi kikubwa udhaifu wa nchi dhidi ya shinikizo la nje na athari za kupoteza viongozi wakuu.

Mtafiti huyo wa Russia alibainisha kuwa:

“Bila shaka, mkakati wa ‘kuangalia Mashariki’ wa Ayatullah Khamenei ulichangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uhusiano wa Iran na Russia pamoja na washirika wengine wasio wa Magharibi.”

Aliendelea kusema kuwa:

Aidha, chini ya uongozi wa Ayatullah Khamenei, Iran imeongeza kwa kiwango kikubwa uwezo wake wa kijeshi na kuweka mkazo maalum kwenye mbinu za vita zisizo za moja kwa moja.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Mufti na Mwenyekiti wa Baraza la Kidini la Waislamu wa Russia amesema kuwa, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kiongozi shahidi wa Iran, wakati wa uhai wake alichukua hatua kubwa katika kuimarisha umoja na maelewano kati ya madhehebu ya Kiislamu.

Mufti Albir Khazrat Krganov amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na kueleza kwamba, baadhi ya watu katika nchi za Magharibi, hususan wataalamu wa masuala ya Uislamu, katika miongo ya hivi karibuni wamejitahidi kuibua mgawanyiko mkubwa kati ya Waislamu wa Sunni na Shia na kuonyesha tofauti hizo kana kwamba, ni ukuta usioweza kuvukwa, ilhali kwa hakika hali si hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *