
Jeshi la anga limetangaza uchunguzi kufuatia shambulio la anga lililoikumba soko huko Jilli, kaskazini mashariki mwa Nigeria, siku ya Jumamosi, Aprili 11. Viongozi wengi, hasa kutoka upinzani, walilaani shambulio hilo la kijeshi, ambalo liliwalenga wanachama wa ISWAP. Ukosoaji huu ulipingwa na ofisi ya Rais Bola Ahmed Tinubu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Abuja, Moïse Gomis
Miongoni mwa ukosoaji mkali ulitoka kwa Makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar. Mpinzani mkuu huyu wa Rais Bola Tinubu alielezea wasiwasi wake kuhusu vifo vya raia wakati wa operesheni dhidi ya Boko Haram na ISWAP.
Tangu mwaka 2017, wachambuzi kadhaa wa usalama wameandika takriban matukio zaidi ya ishirini ambapo raia wameathiriwa na mashambulizi ya jeshi la anga.
Hata hivyo, Sunday Dare, mmoja wa washauri wa Rais Tinubu anayehusika na masuala ya vyombo vya habari na mawasiliano ya umma, analaani mashambulizi ya anga katika mji wa Jilli kutumiwa kisiasa. Kulingana na mshauri huyu wa mkuu wa nchi wa Nigeria, vikosi vya jeshi vinapigana moja kwa moja dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na magaidi. Sunday Dare pia anadai kwamba soko la Jilli limekuwa likishambuliwa kwa miaka mingi na wapiganaji wa Boko Haram na ISWAP, na kwamba soko hili limekuwa kitovu cha vifaa na biashara kwa makundi haya yenye silaha.
Wakati maeneo ya vurugu yakiendelea kuongezeka katika sehemu za kaskazini magharibi na katikati mwa nchi, jeshi la Nigeria lilijibu haraka kwa kuanzisha uchunguzi wa ndani. Lakini hakuna dalili katika hatua hii kwamba Tume ya Haki za Binadamu ya Nigeria inahusika au itahusika katika zoezi hili la uchunguzi kwa mianaji ya kujua ukweli.