
Vyanzo kutoka kwenye jeshi na asasi nyengine za kiusalama nchini Mali, zimethibitisha kutokea kwa shambulio jengine kwenye Miji kadhaa pamoja na gereza, shambulio ambalo limetekelezwa na wanajihadi na washirika wao wa Tuareg wanaotaka kujitenga.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashambulio hayo yameripotiwa katika Miji ya Gao, Anefis na Sevare pamoja na kwenye gereza katika eneo la Kenieroba.
Mashambulio hayo yalioanza leo Jumamosi asubuhi, yamejiri ikiwa imepita miezi miwili baada ya mengine yaliosababisha kifo cha Waziri wa ulinzi wa Mali.
Wapiganaji wa Tuareg wamethibitisha kushambulia mojawapo ya Miji ambayo ina kambi ya wanajeshi wa serikali ya Mali na washirika wao mamluki wa Urusi.