Leo Aprili 15, ni miaka mitatu kamili, tangu kuanza kwa vita nchini Sudan kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF, vita ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine zaidi ya Milioni 11 kuyakimbia makaazi yao, katika mzozo ambao Umoja wa Mataifa unasema Sudan imesahaulika na dunia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati Sudanikitimiza miaka mitatu ikiwa kwenye vita, jijini Berlin nchini Ujerumani, wafadhili na wahisani wa Kimataifa wanakutana kwenye kongamano la kuhimiza amani na kupata fedha za kuwasaidia mamilioni ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu, kama chakula, dawa, makaazi na dawa.

Katika kongamano hili, jeshi na wanamgambo wa RSFwanaopigana hawajaalikwa, na linakuja baada ya makongamano mengine kufanyika jijini London na Paris kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, ambayo yalishindwa kumaliza vita hivyo kwa njia za kidiplomasia.

Tangu kuanza kwa mwaka wa 2026, takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, raia wa Sudan zaidi ya 700 wameuawa katika vita hivyo, hasa Kusini kwa jimbo la Kordofan na Blue Nile.

Licha ya vita kuendelea, Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa watu wengine waliokuwa wameyakimbia makaazi yao, wamerejea katika jiji kuu Khartoum.

Jitihada za kidiplomasia zinazoongozwa na Marekani,Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Misri hazijafua dafu.Saudi Arabia,Misri na Uturuki zinadaiwa kuliunga mkono jeshi la Sudan huku nchi ya Falme ya Kiarabu ikishtumiwa kuwapa silaha RSF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *