
Hoteli ya Carlton-Ritz inapatikana katikati ya hifadhi ya Masai Mara, ambayo pia ndiyo njia ya uhamiaji mkubwa zaidi wa mamalia wa nchi kavu. Baada ya rufaa ya awali dhidi ya mradi huo kukataliwa, wanaharakati wa Kenya wamezindua changamoto mpya ya kisheria ya kuzuia ujenzi zaidi na kutangaza majengo yaliyopo kuwa kinyume cha sheria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kila mwaka, nyumbu milioni mbili, pundamilia, na swala huvuka hifadhi wakati wa uhamaji wa kila mwaka wa wanyama. Hazina ya ikolojia inatishiwa na hoteli hii ya kifahari.
Gichochi Waweru, wakili wa Kenya anayeongoza kesi hiyo, anasema kwamba “sifa za ikolojia za hifadhi hii zinaathiriwa sana na ujenzi huu ambao haujadhinishwa.” Hifadhi ya Masai Mara “haiwezi kuchukua miradi mingine zaidi kwa sasa. Ndiyo maana lazima tupambane ili kulinda uadilifu wa hifadhi.”
Hata hivyo, eneo la ujenzi lilitakiwa kulindwa. Mashirika ya haki za mazingira yaliyo nyuma ya kesi hiyo yanalaani mradi huo kuwa haramu na unafanywa bila kushauriana. “Hatupingi uwekezaji wa kimataifa,” anaeleza wakili Gichochi Waweru. “Hatuna uaduia na Carlton Ritz au wengine. Tatizo ni kuheshimu sheria. Ni suala la uwajibikaji. Hilo ndilo tunalofanya. Tuko mahakamani kuhakikisha kwamba inaheshimiwa.”
Mamlaka ya hifadhi haijajibu chochote. Kujibu shutuma za awali, walibainisha kwamba mradi huo hautaathiri bioanuwai.