
KAIMU Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Patrick Kipangula, amewakumbusha waandishi wa habari kuzingatia maadili ya taaluma yao ili kulinda amani na mshikamano wa jamii.
Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Idara ya Habari ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Kipangula amesema kuwa uandishi usiozingatia maadili unaweza kusababisha athari kubwa kwa jamii. SOMA: Vijana Waibeba Ajenda ya Amani
Amesisitiza umuhimu wa kuripoti kwa tahadhari masuala nyeti, yakiwemo migogoro ya kisiasa, kikabila na kidini, akibainisha kuwa taarifa zisizoandaliwa kwa umakini zinaweza kuchochea migogoro na kuleta madhara makubwa.