
Nchini Burkina Faso, Waziri wa mambo ya aNadani na Uhamaji ametangaza siku ya Jumartano, Aprili 15, 2026, kufutwa kwa mashirika takriban 100. Mamlaka zimetaja kutofuata masharti ya kisheria yaliyopo, bila kutoa maelezo zaidi. Hatua hiyo ilianza kutumika mara moja: mashirika haya hayaruhusiwi tena kufanya kazi kote nchini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchini Burkina Faso, mashirika 118 yanakabiliwa na marufuku hii. Mengi yanahusika katika utetezi wa haki za binadamu. Waziri wa Mambo ya Ndani alionya kwamba shirika lolote litakaloshindwa kufuata hatua hii litakabiliwa na vikwazo, kwa mujibu wa sheria.
Uamuzi huu unaangukia ndani ya mfumo wa sheria iliyopitishwa mwezi Julai 2025, ambayo inadhibiti kwa ukali zaidi uhuru wa kujumuika, pamoja na majukumu ya kiutawala na kifedha yaliyoimarishwa. Kulingana na mamlaka, inalenga “kusafisha” sekta hiyo na kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi.
Sheria hiyo ilipopitishwa, Bunge lilitoa muda wa mwaka mmoja kwa mashirika kuzingatia kanuni mpya, kuanzia kuanza kutumika kwake Julai 23, 2025. Hata hivyo, muda mfupi baadaye, mashirika 21 yasiyo ya kiserikali yalinyang’anywa leseni zao za kufanya kazi.
Mapema mwezi Aprili, serikali pia ilitishia kuchukua “hatua kali” dhidi ya kile inachokiita “mashirika ya kibeberu yaliyojificha kama mashirika yasiyo ya kiserikali,” siku chache baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch ikishutumu ukiukwaji wa haki za binadamu unaohusishwa na jeshi.