Mwanasheria wa zamani wa klabu ya Yanga SC na wakili wa FIFA pamoja na International Criminal Court, Simon Patrick, ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya AFCON.

Uteuzi huo umefanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Simon Patrick anakuja na uzoefu mkubwa katika masuala ya sheria za michezo na kimataifa, jambo linalotarajiwa kuongeza nguvu katika kamati hiyo muhimu. Akiwa amewahi kuhudumu katika taasisi kubwa za kimataifa kama FIFA na ICC, uteuzi wake unaonekana kuwa chachu ya mafanikio katika maandalizi ya AFCON.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *