Serikali imetoa vitendea kazi vyenye thamani zaidia ya Shilingi Bilioni 1, kwa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Lindi kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi kupitia Shirika hilo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Tellack akipokea vifaa hivyo ikiwemo magari, bajaji, pikipiki na Komputa anasema vifaa hivyo ni nguzo muhimu ya kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati, huku akieleza kuwa Mkoa wa Lindi upo mbioni kupata umeme wa uhakika kutokana na kazi kubwa inayoendelea sasa ya kuunganishwa kwenye gridi ya taifa.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)