Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na UN Women, kutokea jijini Cairo, Misri, Geneva Uswisi na New York, Marekani imeeleza kuwa hata baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kutangazwa mwezi Oktoba 2025, ripoti zinaonesha kuwa mauaji ya wanawake na wasichana yameendelea kuripotiwa katika miezi ya hivi karibuni, jambo linalothibitisha kuwa tishio dhidi ya maisha yao bado ni kubwa.

Ripoti hiyo yenye jina la “Gharama ya Vita vya Gaza kwa Wanawake na Wasichana”, imefafanua kuwa takriban wanawake na wasichana 11,000 wamepata majeraha yaliyosababisha ulemavu wa maisha.Hata hivyo, idadi halisi ya waaathirika inahofiwa kuwa kubwa zaidi kwa sababu miili mingi imenaswa chini ya vifusi, huku mfumo wa taarfa za afya ukiwa umeporomoka na kuzuia uwekaji wa kumbukumbu sahihi za vifo na majeraha.

Hali hii imeacha makovu makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa waliobaki hai ambao sasa wanapaswa kuanza maisha upya katikati ya uharibifu.

Mkurugenzi wa UN Women katika Kanda ya nchi za Kiarabu, Moez Doraid, amesema, “Athari za vita kwa wanawake na wasichana zimekuwa za kutisha. Pamoja na idadi kubwa ya vifo, vita vimebadili muundo wa familia, huku makumi ya maelfu ya kaya sasa yakiwa yanaongozwa na wanawake. Wengi wanakabiliana na changamoto za kiuchumi zilizoongezeka na hatari kubwa wakati wakibeba mzigo mzima wa malezi na kuendelea kuishi.”

media:entermedia_image:9fa685b2-8c69-4b87-93e2-c0f2d0648655

Wasichana vigori katika ukanda wa Gaza.

Wanawake na wasichana waheshimiwe

Bwana. Doraid ametoa wito wa kutekelezwa kikamilifu kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

“Tunahitaji kuona makubaliano ya kusitisha mapigano yakitekelezwa kikamilifu, kukiwa na uzingatiaji kamili wa masharti yake, kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa, kuimarishwa kwa uwajibikaji, na ulinzi wa wanawake na wasichana pamoja na misaada ya kibinadamu inayotolewa kwa kiwango kikubwa bila vikwazo. Wanawake na wasichana lazima wawe katikati ya juhudi za hatua za urejeshaji wa hali ya kawaida, pamoja na ushiriki wenye tija katika ujenzi wa amani na ujenzi mpya,” ameongeza Doraid.

UN Women imeendelea kubaki Ukanda wa Gaza ikishirikiana na mashirika ya kutetea haki za wanawake kwa kutoa ufadhili, uratibu, na msaada wa kitaalam.

Kwa kushirikiana na mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa na washirika wa kibinadamu, shirika hilo limekuwa likijitahidi kuwafikia wanawake na wasichana kwa misaada ya kuokoa maisha.

Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa sauti za wanawake zinasikika na uwakilishi wao unakuwepo katika juhudi zote za ujenzi mpya ili kurejesha utu na matumaini kwa wakazi wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *