
Jeshi la Iran limesema limefunga tena mlango wa bahari wa Hormuz kutokana na kile limekitaja kama hatua ya jeshi la Marekani kuendelea kuzuia meli zinaoingia na kutoka kwenye bandari za Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais Trump jana alikaribisha hatua ya Iran kufungua mlango huo lakini akasisitiza kwamba nchi yake itaendelea kuzuia meli za Iran hadi pale mkataba wa amani utakapopatikana.
Katika taarifa yake kupitia televisheni inayomilikiwa na serikali, jeshi la Iran limesema Washington imevunja ahadi yake kwa kuendelea kuzuia meli zinazoingia nakuondoka katika bandari ya Iran.
Kulingana na Iran, Hormuz imefungwa tena hadi pale ambapo Marekani itaruhusu meli zinazoingia na kutoka Tehran kusafiri kwa uhuru bila vikwazo.