Serikali imepiga marufuku mikusanyiko yote ya umma katika mji mkuu  wa Kinshasa, na pia katika mikoa ya Tshopo, Haut-Uele, na Bas-Uele. Hatua hii inalenga kupunguza kuenea kwa virusi vya Ebola, kulingana na taarifa rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umechukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Jacquemain Shabani, katika taarifa iliyoelekezwa kwa magavana wa mikoa iliyoathiriwa siku ya Jumamosi, Juni 27.

Waziri alielezea kwamba kizuizi hiki kinakuja katika muktadha wa hatari kubwa ya kiafya inayohusishwa na mzunguko wa virusi vya Ebola katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Serikali inabaini kwamba msongamano wa watu wanaotoka eneo moja kwenda lingine, pamoja na ukaribu wa mikoa na maeneo yanayoweza kuwa na mlipuko huo, kunaweza kuharakisha maambukizi ya virusi hivyo.

Mikutano na maandamano ya umma yamesitishwa

Taarifa hiyo inabainisha kuwa aina zote za mikusanyiko ya watu wengi sasa zimepigwa marufuku katika mikoa manne iliyoathiriwa

  • Mikusayiko iliyopigwa marufuku:
  • Mikutano ya kisiasa,
  • Mikusanyiko na maandamano ya umma,
  • Pamoja na mikusanyiko mingine yoyote inayoweza kuwakusanya watu wengi.

Kwa mamlaka, hatua hii inalenga hasa kupunguza kutangamana kati ya raia ili kupunguza kuenea kwa virusi.

Upinzani unalaani uamuzi ulio “kinyume na katiba”

Upinzani unauita uamuzi huu kinyume cha katiba, ukiamini “ulibuniwa katika maabara ya UDPS,” chama cha rais ambacho Waziri wa Mambo ya Ndani ni mfuasi wa chama hicho.

Prince Epenge, msemaji wa muungano wa Lamuka, anadai kwamba hatua hii inalenga mahususi maandamano yaliyotangazwa na muungano wa C64, yaliyopangwa kufanyika Julai 8, yaliyokusudiwa kuelezea kutokubaliana kwake na majaribio ya walio wengi, kambi ya rais, ya kurekebisha Katiba.

Marekebisho haya ya katiba yanaweza kufungua njia kwa muhula wa tatu kwa rais wa sasa, Félix Tshisekedi, ambaye muhula wake wa sasa unamalizika rasmi mwezi Desemba 2028.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *