Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota, ameitaka Serikali kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa gesi majumbani akieleza kuwa hadi sasa idadi ya wananchi wanaonufaika na huduma hiyo bado ni ndogo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo.

Amesisitiza umuhimu wa kupanua miundombinu ya mabomba ya gesi akibainisha kuwa upanuzi huo unapaswa kufanyika kutoka Mtwara kupitia Nanyamba, Tathaimba hadi Newala na Masasi, ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wa maeneo ya ndani wanapata nishati hiyo muhimu kwa matumizi ya nyumbani na shughuli za kiuchumi.

Aidha, Chikota ameizungumzia changamoto ya upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara, akieleza kuwa suluhisho la kudumu ni kuunganisha kikamilifu mikoa hiyo kwenye gridi ya taifa ili kuondoa matatizo ya mara kwa mara ya umeme na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *