Watu 14 waliokuwa kwenye ndege ya abiria, wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kuanguka nchini Sudan Kusini, baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Yei, kuelekea jiji kuu Juba.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ndogo aina ya  Cessna 208 inayomilikiwa na kampuni ya  CityLink Aviation ilianguka takriban kilomita 20  kusini-magharibi mwa mji mkuu, Juba, Jumatatu asubuhi,baada ya  udhibiti wa trafiki wa anga  kupoteza mawasiliano  takriban dakika 30 baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Yei.

Miongoni mwa watu  waliokuwa ndani ya ndege hiyo  ni rubani na abiria 14 , 13 wakiwa raia wa sudan kusini  na Wakenya wawili.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa ajali hiyo huenda ilisababishwa na hali mbaya ya hewa, hasa kutoonekana vizuri,wakati huu  kikosi cha kuchunguza ajali za ndege kikitumwa kwenye ĂȘneo la ajali hiyo kwa uchunguzi zaidi .

Katika kipindi cha muongo mmoja Zaidi ya ndege 55 zilianguka nchini humo na kusababisha vifo vya watu kadhaa nyingi za ajali hizo zikisababishwa na hali mbaya ya hewa na hali duni ya kuratibu safari za ndege nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *